Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Juventus Paul Pogba, 23, na wametoa dau la pauni milioni 86 (Daily Mail), Manchester City watamfuatilia Riyad Mahrez, 25, ikiwa watashindwa kumpata winga wa Schalke Leroy Sane, 20 (France Football), Atletico Madrid watamgeukia mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, 21, iwapo watashindwa kumpata Diego Costa, 27 kutoka Chelsea (Bleacher Report), Barcelona wako tayari kumuuza kiungo wao Arda Turan, 29, kwa pauni milioni 20, huku Chelsea na Arsenal zikimtaka mchezaji huyo (Talksport), meneja wa Stoke City Mark Hughes amethibitisha kuwa klabu yake imepanda dau kwa West Brom kumtaka mshambuliaji mwenye asili ya Burundi, Saido Berahino, 22, lakini bado hawajapata majibu yoyote (Sky Sports), Stoke pia wanamtaka mshambuliaji Jose Angulo, 21, anayechezea Independente ya Ecuador (Guardian), Manchester City na Manchester United zote zinamtaka beki wa West Ham Reece Oxford, 17, ambaye thamani yake ni pauni milioni 15 (Sky Sports), Crystal Palace wanamtaka mshambuliaji wa West Ham, Diafra Sakho, 26 kwa pauni milioni 15 (Daily Mirror), Manchester United wanafikiria kutoa dau la pauni milioni 25 kumsajili beki kutoka Brazil Fabinho, 22, anayechezea Monaco (Daily Mail), Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa kipa kutoka Argentina Geronimo Rulli, 24, kwa pauni milioni 4 (Guardian), Liverpool wamekuwa na mazungumzo na Newcastle kuhusu kumsajili kiungo wa Newcastle na Uholanzi, Giorginio Wijnaldum, 25, ambaye thamani yake ni pauni milioni 27 (Newcastle Chronicle), Newcastle United huenda wakataka kumsajili kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29, kama sehemu ya uhamisho wa Wijnaldum (Telegraph), meneja wa Manchester United yuko tayari kuwaachilia beki Tyler Blackett, 22, na washambuliaji Will Keane, 23, na James Wilson, 20 kuondoka Old Trafford (Daily Telegraph), Besitkas ya Uturuki itamfuatilia mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy, 29, iwapo watashindwa kumpata Mario Gomez, 31 anayecheza Fiorentina (Evening Standard).
Credit:Salim Kikeke
0 comments:
Post a Comment