Saturday, July 23, 2016

Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte amemuambia mmiliki wa timu Roman Abramovic kuwa anahitaji kusajili wachezaji wengine watano ili Chelsea irejee katika ubora wake (Daily Mirror), Manchester United wanafikiria kutoa dau la pauni milioni 54 kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez, 25 (El Confidencial), Manchester City watarejea tena Everton na kutoa dau la zaidi ya pauni milioni 50 kumtaka beki John Stones, 22 (Daily Mirror), meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino amewaacha Nabil Bentale, 21, Clinton N’Jie, 22, Federico Fazio, 29, na Alex Pritchard, 23, katika kikosi kilichokwenda Australia, na huenda wakauzwa (The Sun), kiungo wa Liverpool, Lucas Leiva, 29, anasakwa na Galatasaray ya Uturuki (Daily Mail), meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekatishwa tamaa ya kumsajili kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos, 24, kwa sababu ya mshahara wa pauni 240,000 kwa wiki wa mchezaji huyo (The Sun), Ryan Giggs na Roy Keane wanatajwa kuziba nafasi ya Steve Bruce aliyeondoka Hull City (Daily Express), meneja wa Leicester Claudio Ranieri amesema beki wa kushoto Ben Chilwell, 19, atasaini mkataba mpya, kufuatia tetesi kuwa Liverpool wamepanda dau la pauni milioni 7 (Leicester Mercury), mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli, 25, anahitaji ”nafasi nzuri” ili kurejea katika ubora wake, amesema wakala wake Mino Raiola (Liverpool Echo), Everton wanajiandaa kutoa pauni milioni 25 kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 26 (Daily Express), West Brom wametoa dau la pauni milioni 7 kumtaka beki wa Brighton Lewis Dunk, 24 (Daily Mirror), mshambuliaji wa Arsenal amemshawishi meneja Arsene Wenger kumsajili kiungo wa Barcelona Arda Turan, 29 (The Sun), Arsenal pia huenda wakakasirisha mashabiki wao tena baada ya kusema wasitarajie usajili wowote wa bei ghali msimu huu (The Times).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video