Chelsea wanafikiria kutoa dau la takriban pauni milioni 50 kumsajili tena Romelu Lukaku, 23, kutoka Everton. Everton wanasema Lukaku ana thamani ya pauni milioni 65 (Liverpool Echo), Manchester City wapo katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Palmeiras, Gabriel Jesus, 19, ambaye pia anasakwa na Barcelona, Real Madrid na Manchester United (Manchester Evening News), Tottenham watampa mkataba mpya wa miaka mitano kiungo Eric Dier, 22, na kumpa mshahara wa pauni 70,000 kwa wiki (Telegraph), iwapo kiungo wa Juventus atakwenda Manchester United, wakala wake huenda akalipwa pauni milioni 20 (Daily Mail), wakala mwenyewe Raiola anakanusha kuwa mkataba wa Pogba tayari umekamilika (The Sun), Chelsea wameambiwa walipe pauni milioni 67 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata, 23 (Daily Mirror), matumaini ya West Ham ya kumpata Mario Gomez, 31, yameongezeka baada ya mshambuliaji huyo kusema anaondoka Besitkas (daily Express), Chelsea watatoa pauni milioni 41.61 kumsajili Edinson Cavani (le 10Sport.com)
Friday, July 22, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment