Sunday, July 10, 2016

Uongozi wa Klabu ya Stand United ya Mjini Shinyanga inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA Jana ulikua na mkutano na wajumbe wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) kwaajili ya uthibitisho wa uhalali wa klabu ndani ya shirikisho la soka nchini ukiwa na lengo la kutatua sintofahamu juu ya uhalali wa klabu.

Mkutano wa jana ulikua chini ya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wakili msomi Revocatus Kuuli na Mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya TFF Hamimu Omary Agenda kuu ikiwa ni kujiridhisha uhalali wa  uwanachama wa Stand united ndani ya TFF

Haya ndiyo mambo yaliyofanywa na Wakili Kuuli

 1. Alihakiki wanachama na Muhtasari uliyosajili wanachama 33 na wengineo 19 jumla wakifikia wanachama 52 ambao ni wachama halali wa Stand United na katika hao wanachama wawili walishafariki dunia hivyo Stand United kubaki na wanachama 50.
Kati ya wanachama hao 30 ni waanzilishi wa timu ya Stand United na katika hao 24 walikuwepo katika mkutano huo na 6 tu hawakuwepo kutokana na shughuli zao za kikazi wakitoa udhuru kabla.
Alipitia pia Muhtasari wa usajili wa Stand united uliambatanishwa na majina ya wanzilishi pamoja na cheti cha usajili wa timu ya Stand United.

Baada ya hapo uhakika wa wanachama wengine uliendelea na kila mwanachama alikuwepo kwa maana hiyo Wakili Msomi Kuuli na mwenzake Hamimu walijiridhisha kwamba Stand United ni nani na wanapatikana wapi. Wakitumia muda huo kupiga picha wanachama wote wakiwa na vitambulisho vyao na kadi za uanachama.

 Zoezi la pili lilikuwa ni kuhakiki mstakabali wa Stand United kuwa kampuni na kama mchakato huo ulikuwa na baraka za wanachama wote. Baada ya kupitia Nyaraka zote za usajili wa Stand United Company Limited wanachama wote kwa sauti moja walikiri na kuitaarifu kamati ya Wakili msomi Kuuli kwamba huo ni mchakato uliopitishwa na wanachama wote wa Stand United na kwamba wanahisa wote walikubali timu kuwa kampuni. 

Baada ya hapo Wakili Kuuli alienda upande wa pili ili kujiridhisha kama na wenzetu wale wana nyaraka tulizonyesha na udhabiti wa wanachama wao.

HITIMISHO
Kwa kifupi mtu atakuwa mwanachama wa Stand United kama atafata utaratibu unaonyeshwa katika Ibara ya 7 na 8 ya katiba ya Stand united na awe na kadi ya Stand United. 
Tunasikita kusikia vyombo vya habari vinavyotangaza kuwa kundi flani limepewa ushindi na wakili Kuuli ilhali maamuzi kamili ya hayajatolewa.
Asanteni
Imetolewa na 
ALEXANDER SANGA 
MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO 
STAND UNITED COMPANY LIMITED 
0715052491

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video