Usiku wa Jumapili Julai 16 zimetolewa tuzo kwa timu, wachezaji na makocha kutokana na kufanya vizuri kataika ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa 2015/16 ambao ulimalizika mwezi Mei kwa Yanga kuibuka mabingwa na kutwaa taji lao kwa mara ya 26 katika historia.
Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.
Kwenye mabano ni kiasi cha fedha ambacho washindi wa tuzo wamepata kutoka kwa mdhamini wa ligi Tanzania bara, tuzo zilitolewa kwa washindi kama ifuatavyo,
- Mshindi wa nne: Tanzania Prisons (Tsh.23,241,635)
2. Mshindi wa tatu: Simba SC (Tsh. 29,052,044)
3. Mshindi wa pili: Azam FC
4. Bingwa wa ligi kuu 215/16: Yanga SC (Tsh. 40,672,861)
5. Mfungaji bora wa msimu wa 2015-16: Amis Tambwe Tsh. 5,742,940)-alifunga magoli 21 magoli mawili mbele ya mpinzani wake Hamisi Kiiza aliyefunga magoli 19
Walioingia katika kinyang’anyiro hicho ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope.
- Goli bora la msimu: tuzo imekwenda kwa Ibrahimu Ajib (Simba)
- (Tsh. 3,000,000)
Ajib alikuwa akipambana na Amis Tambwe (Yanga) katika kuwania tuzo ya goli bora la msimu 2015-16.
- Golikipa bora ni Aishi Manula (Azam FC) (Tsh. 5,742,940)
Majina yaliyopendekezwa kuwania tuzo hiyo ni Aishi Manula (Azam)Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).
- Kocha bora wapo Hans Van Pluijm (Yanga (8,000,000)
Waliokuwa wakipambana kuwania tuzo ya kocha bora wa msimu uliopita ni Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons).
- Mchezaji bora wa kigeni ni Thabani Kamusoko (Yanga) (Tsh. 5,742,940)
Waliongia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba).
- Mchezaji bora chipukizi ni Mohamed Hussein (Simba) (Tsh. 4,000,000)
Waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).
- Mchezaji bora wa Ligi ni Juma Abdul (Yanga) (9,228,820)
Waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi walikuwa ni Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na Mohamed Hussein (Simba).
0 comments:
Post a Comment