Mbwana Samatta leo anatarajiwa kuonekana tena katika nyasi za Ulaya pale timu yake ya Genk itakapovaana na KV Oostende katika muendelezo wa mechi za ufunguzi katika Ligi Kuu ya Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro League.
Mchezo ambao utachezwa kunako dimba la Cristal Arena, nyumbani kwa Genk utaanza saa 1 kamili za usiku kwa majira ya Tanzania na Afrika Afrika Mashariki kwa ujumla.
Ikumbukwe tu, huu ndio msimu ambao Samatta anaanza kuanzia mwanzo mara baada ya msimu uliopita kuukuta mwishoni kufuatia ksajiliwa katika dirisha dogo akitokea TP Mazembe ya DRC.
Samatta, akiwa kama miongoni mwa washambuliaji tegemezi tayari alibainisha dhamira yake tangu mwanzo kwamba anataka kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, hivyo ni jukumu lake sasa kuhakikisha msimu huu timu yake inafanya vizuri ili kukamilisha ndoto zake.
Msimu uliopita, Samatta aliwafunga Oostende katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi waliyokutana, hivyo kumbukumbu hii ni morali tosha ya kuhakikisha anaisaidia tena timu yake kuibuka na ushindi leo.
Genk na Oostende wamekutana mara kumi katika michuano tofauti-tofauti. Oostende anaonekana kuwa na rekodi nzuri zaidi baada ya kufanikiwa kushinda michezo 4, huku Genk wakishinda mara 3 na kutoka sare mara tatu.
Msimu uliopita Genk walimaliza nafasi ya tano baada ya kujikusanyia alama 48 huku Oostende wakimaliza nafasi ya nne baada ya kupata alama 49.
0 comments:
Post a Comment