Licha ya kuhisiwa kupata maumivu makubwa ya goti, Cristiano Ronaldo anaonekana kutokufikiria sana kuhusu jeraha hilo. Kwa sasa anaonekana kusherehekea kwanza ubingwa wa Euro ambao ni moja ya makombe aliyokuwa akiyahusudu kwa muda mrefu sana kwenye maisha yake ya soka. Licha ya kuwa muda mwingi alikuwa nje ya uwanja lakini mchango wake ulionekana.
Lakini taarifa za uchunguzi wa jeraha lake zinadai kwamba, Ronaldo anamepata mapasuko wa mfupo kwenye eneo la goti na inawezekana kwa kiasi kikubwa akakaa nje ya uwanja kwa takriban miezi minne mpaka mitano
Vitu gani hasa Ronaldo atakosa ikiwa atakaa nje kwa muda huo.
Kama ripoti hizi zinathibitishwa rasmi, basi Ronaldo atakuokosa mchezo wa UEFA Super Cup Agosti 9. Pia atakosa michezo lukuki ya La Liga na michezo ya Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi
Ronaldo alifunga goli muhimu lililoipa ubingwa Real Madrid kwenye changamoto ya mikwaju ya penati kwenye fainali ya Uefa dhidi ya Atletico mwezi May.
Kwenye michuano hiyo aliibuka mfungaji bora akiwa na magoli 16.
0 comments:
Post a Comment