Robo fainali ya nne ya Michuano ya Euro inaendelea tena leo ambapo wenyeji Ufaransa watakuwa na kibarua kigumu mbele ya wabishi wa Iceland, mchezo utakaopigwa kunako dimba la Stade de France lililopo jimbo la Saint-Denis jijini Paris.
Taarifa za kila timu
Beki wa Ufaransa ambaye hajacheza hata mchezo mmoja kwenye michuano hii Samuel Umtiti anatarajia kuchukua mikoba ya Adil Rami ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano, wakati kiungo N'Golo Kante atakuwa pia akitumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja.
Ufaransa watakuwa wakitumia mfumo wa 4-3-3 ambao walianza nao katika mchezo dhidi ya Jamhuri ya Ireland huku Yohane Cabaye akitarajiwa kubeba mikoba ya Kante mwenye kadi mbili za njano.
Lakini endapo Ufaransa wataamua kubadili mfumo, basi Kingsley Coman au Moussa Sissoko wanweza kupata nafasi ya kuanza.
Kikosi cha Iceland kinaweza kisiwe na mabadiliko yoyote, huu ukiwa ni mchezo wa tano mfululizo kufanya hivyo.
Wachezaji tisa wa Iceland wana kadi za njano na hivyo endapo watapata nyingine tena leo maana yake wataukosa mchezo wa nusu fainali ebdapo timu yao itafuzu.
Olivier Giroud na Laurent Koscielny wote wana kadi za njano, wanahitaji tahadhari kubwa kuepeka kadi nyingine zitakazowazuia kucheza mchezo wa nusu fainali ikiwa tu Ufaransa itafuzu.
Uchambuzi mfupi kuelekea mchezo huu.
Kama ambavyo imetokea kwa Wales ambao wanashiriki kwa mara yao ya kwanza michuano hii na kutinga nusu fainali baada ya kuwatupa nje Ubelgiji, wenzao Iceland ambao pia wanashiriki kwa mara ya kwanza wanaweza kufanya maajabau na kuufanya mwaka huu kuwa wa timu ngeni tena zilizokuwa hazipewi nafasi kubwa katika michuano hii.
Wales walisema kwamba ushindi wa kushtua wa Iceland dhidi ya England uliwapa morali kubwa na kupelekea kufanya makubwa Ijumaa kwa kuwatupa nje ya mashindano Ubelgiji.
Kocha wa viungo wa Iceland Heimir Hallgrimsson anatumaini kwamba timu yake itafuata mfano wa Leicester City, baada ya kuchukua ubingwa pasopo matarajio ya wengi. "Ningependa tumalize kama walivyomaliza Leicester," alsema.
"Walicheza kwa juhudu zao zote na sisi pia tunajitahidi kucheza kwa juhudi zetu zote. Kuna morali na ari inayofanana kwa timu zote mbili. Tuko tayari kufanya kazi kwa pamoja.
Ufaransa wamekuwa na heshima kubwa kuelekea mchezo huu. Nahodha wao Hugo Lloris amesisitiza kwa kusema "Tunatambua kwamba kuwa taifa linalocheza soka la kuvutia haitoshi tu kuwafanya mfike hatua ya nusu fainali."
"Timu bora zinazocheza soka zuri hazipo tena hapa," aliongeza.
"Hii inaonyesha ni dhahiri tunapaswa kucheza kitimu ili kupata matokeo. Ni uimara wa fikra ndiyo unaleta utofauti na hivyo ndivyo namna tunavyohitaji kufanya ili kuweza kufuzu.
"Hakutakuwa na mshangao wowote kwetu, kama tunaenda uwanjani na kujiamisha kwamba sisi ni bora na tuna vipaji zaidi, na kutofanikiwa."
Takwimu za michezo waliyowahi kukutana
- Ufaransa hawajapoteza dhidi ya Iceland kwenye michezo 11 iliyopita, kati ya michezo hiyo wameshinda nane.
- Iceland wamepoteza michezo yao yote sita ya ugenini dhidi ya Ufaransa, wamefunga magoli matano na kufungwa 22.
- Katika michezo yao miwili ya mwisho, Ufaransa waliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
- Mchezo pekee ambao Iceland walicheza kunako dimba la Stade de France ilikuwa ni mwaka 1999 kwa ajili ya kufuzu michuano ya Euro mwaka 2000. Iceland walitoka nyuma kwa magoli 2-0 na kufungwa magoli 3-2, shukrani za dhati ziende kwa David Trezeguet aliyefunga goli la ushindi kwa Ufaransa na Eidur Gudjohnsen ambaye alitokea benchi kwa upande wa Iceland na kufanya makubwa uwanjani.
Ufaransa
- Huu unakuwa ni mchezo wa 80 kwa Ufaransa kucheza kunako dimba la Stade de France (wameshinda mara 49, droo ishirini na kufungwa mara 10).
- Wameshinda michezo minne kati ya mitano katika michunao mbalimbali mikubwa. Mchezo wao waliotoka suluhu ulikuwa dhidi ya Italy kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1998. Walishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
- Hii ni michuano ya tatu mfululizo ambayo Ufaransa wamefanikiwa kufuka robo fainali. Kwenye hatua kama hii walipoteza kwenye michuano ya Euro 2012 na Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Uhispania na Ujerumani mtawalia.
- Kwenye michuano minne iliyopita Ufaransa waliondolewa kwenye hatua kama hii katika michuano mikubwa mbalimbali, timu ilikuwa ikiwatoa ilienda kubeba kombe. Timu hizo ni Italy na Ujerumani kwenye Kombe la Dunia mwaka 1938 na 2014, na Ugiriki na Uhispania kwenye mMichuano ya Euro mwaka 1938 and 2014.
- Hawajafungwa kwenye michezo yao 16 iliyopita katika michuano tofauti-tofauti katika ardhi ya nyumbani, wameshnda 14 na kutoa sare miwili.
- Ufaransa wameruhusu magoli mawili kwa penati kwenye Michuano ya Euro mwaka huu lakini hawafungwa goli lolote kwa njia ya kawaida.
- Kwenye michuano ya mwaka huu, wameruhusu wapinzani wao kupiga jumla ya mashuti matatu tu yaliyolenga lango, machache zaidi kuliko timu yoyote. Mawili kati ya hayo dhidi ya Romania na Jamhuri ya Ireland yalikuwa ni kupitia penati.
- Antoine Griezmann amefunga magoli matatu kwenye michezo minne iliyopita lakini hajawahi kuifungia goli Ufaransa pindi wakicheza kwenye uwanja wa Stade de France (amecheza kwa dakika 603).
Iceland
- Magoli yote sita ya Iceland kwenye Michuano ya mwaka huu yamefungwa na wachezahi tofauti-tofauti.
- Michezo yao yote minne waliyocheza nchini Ufaransa timu zote zilipata magoli.
- Iceland imepoteza mara moja tu kwenye michezo yao ya ushindani 10 iliyopita (wameshinda mitano, sare minne).
- Ni moja kati ya timu mbili ikiwemo Wales kuweza kufunga kwenye michezo yake yote ya Euro mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment