Mlinzi wa kati Rajab Zahir aliyekuwa akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Stand United akitokea Dar Young Africans ya jijini Dar es Salaam amejiunga na kikosi cha Mbeya City Fc leo.
Kwenye ofisi za City zilizopo Mkapa Hall, eneo la Soko Matolla, jijini hapa, Zahir, amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kujunga na kikosi cha kocha Kinnah phiri na kusema kuwa ana imani kubwa ya kupata mafanikio yake kisoka akiwa na chini ya kocha huyo bora kutoka Malawi.
“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kujiunga na City, hii ni moja kati ya timu kubwa nchini kwa sababu ina ushawishi wa kutosha kwenye soka la nchini yetu, kitu muhimu ni kuomba ushirikiano kutoka kwa pande zote kwa maana ya uongozi wachezaji wenzangu na mashabiki, hayo yote yatatufanya kutimiza malengo kwa sababu kila mmoja anahitaji mafanikio katika kazi kwangu mimi hapa ndiyo sehemu ambayo nitayapata” alisema.
Zahir amejiunga na City baada ya msimu mmoja wa mkopo kwa Stand United ya Shinyanga uliohitimisha kandarasi yake ya miaka 3 na kikosi cha Yanga ya Dar es Salaam,
Akiwa Stand United, Zahir alifanikiwa kucheza michezo 23 katika mechi zote 30 zilizochezwa na timu hiyo ya Shinyanga na kufanikiwa kushika nafasi ya 7 ikikusanya jumla ya pointi 40 mwisho wa msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment