Saturday, July 9, 2016

Paul Pogba na Patrice Evra wamekuwa ni watu wenye furaha kubwa hasa baada ya timu yao kufuzu kutinga fainali ya Euro mwaka huu, michuano inayofanyika nchini mwao.
Licha kutopitwa umri mkubwa sana, Pogba amekuwa akimwita Evra ‘Uncle Pat’, kama jina la heshima kutokana na kuzidiwa umri na mkongwe huyo. Wawili hao wote wanacheza kunako klabu ya Juventus.
Wawili hao wote walikuwa kwenye kiwango bora kabisa kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani huku wakitoa mchango mkubwa kwenye ushindi wa timu yao, baada ya mchezo huo waliamua kufanya mahojiano kwa kutumia lugha ya Kiitaliano.
Walipopewa nafasi na mwandishi wa habari wa moja ya vyombo vya habari vya Italy, Pogba na Evra waliamua kuchukua kipaza sauti kujifanyia mahojiano wenyewe.
Pamoja na mambo mengine, Evra na Pogba walichukua nafasi hiyo kumwambia kocha wao wa Juve Max Allegri kwamba wanahitaji mapumziko zaidi kuelekea maandalizi ya msimu mpya kutokana na kukabiliana na mchezo wa fainali.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video