Jana kocha mpya wa Manchester City Pep Guardiola alitambulishwa rasmi kwa mashabiki 7000 wa klabu hiyo kunako dimba la Etihad.
Gaurdiola alilakiwa kwa furaha na mashabiki wa klabu hiyo pamoja na baadhi ya wachezaji walikuwepo wakati wa utambulisho huo.
Leo ameanza rasmi kazi ya kukinoa kikosi hicho huku akionekana ni mwenye bashasha kubwa usoni akiwa kwenye sehemu yake mpya ya kazi.
Miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye mazoezi leo ni pamoja na Yaya Toure ambaye alionekana kuwa na furaha licha ya uhusiano wake na kocha huyo kuwa mashakani kwa kiindi kirefu tangu alipoondoka Barelona.

Pep Guardiola akiondoka uwanjani baada ya kumaliza mazoezi ya siku yake ya kwanza kama meneja wa Manchester City.

Guardiola na jopo lake wakiwapa maelekezo wachezaji wao katika mazoezi yaliyofanyiaka uwanja wa mazoezi karibu kabisa na Etihad

Wachzaji wakipata vinjwaji kabla ya kuendelea tena na mazoezi.

Kocha mpya wa masuala ya fitness Lorenzo Buenaventura akiwafua vijana wake.
0 comments:
Post a Comment