Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon amesaini mkataba wa miaka miwili kuionoa Simba ya Dar es Salaam, mkataba huo utaisha mwaka 2018.
Omog amesaini mkataba huo leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva.
Omog amesema anaujua ukubwa wa Simba na changamoto zake na amesisitiza atapambana kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ingawa amesisitiza suala la muda kwa kuwa kila kitu hakiwezi kubadilika siku moja.
0 comments:
Post a Comment