Thursday, July 21, 2016

Borussia Dortmund wametangaza kumsajili Mario Gotze kutoka Bayern Munich. 
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ambaye alifunga goli la ushindi kwenye Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014, awali alikuwa mchezaji Dortmund na baadaye kusajiliwa na Bayern na sasa kaamua kurudi tena nyumbani. 
Kabla ya kuondoka Dortmund mara ya kwanza, Gotze alikuwa ameifungia timu hiyo mabao 31 kwenye michezo 116 huku mchezo wake wa kwanza kwa klabu hiyo ukiwa ni mwaka 2008. 
Baadhi ya mashabiki walikuwa hawataki Gotze arudi kunako klabu hiyo, lakini tayari ameshathibitishwa kuwa mchezaji wa Borussia mpaka mwaka 2020 baada ya kusaini mktaba wa miaka minne. 
Kiungo huyo mshambuliaji pia amewaomba radhi mashabiki wote wa klabu hiyo na kuahidi kujituma ili kurejea katika ubora wake na kurudisha imani kwa mashabiki wa timu hiyo
 "Wakati nilipotoka BVB kwenda Bayern mwaka 2013 nilifanya maamuzi ambayo nilijua kwamba nafanya nini na kamwe siwezi kuongopa juu ya hili leo.
"Miaka mitatu imepita sasa na nina miaka 24, najitambua kwa kila maamuzi ninayochukua. Natambua wazi kwamba mashabiki wangu wasingeweza kunielewa juu ya maamuzi niliyofanya. Kamwe nisingefanya kitu kama hicho wakati huu!
"Ninarejea nyumbani sasa, Nataka kujaribu kuwashawishi watu juu ya kiwango changu, hasa wale ambao wamezipokea taarifa za ujio wangu kwa shingo upande. Lengo langu kwa mara nyingine ni kucheza kwa nguvu zangu zote. Kwa ajili yetu sote, klabu na mshabiki kwa ujumla. "
Gotze hakuwa na wakati mzuri kwenye klabu ya Bayern huku msimu uliopita akipata mafasi ya kucheza mara 14 tu kwenye ligi ya Bundesliga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video