Aliyekuwa winga wa kuogopwa wa Stand United ya Shinyanga, maarufu Chama la wana, Haruna Athuman Chanongo amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili na Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani, Mkoani Morogoro.
Chanongo alisaini kandarasi hiyo jana mbele ya Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser.
Awali alisaini Stand United upande wa kampuni, ambao tayari TFF imetangaza kutoutambua upande huo na mchezaji huyo, rasmi jana alijiunga na Mtibwa.
Nyota huyo aliyewahi kutamba na Simba SC kabla ya kutolewa kwa mkopo Stand United ambako baadaye alijiunga moja kwa moja, anaingia Mtibwa Sugar huku akiwa na uhakika mkubwa wa kupata namba kutokana na nyota kadhaa muhimu kutimka kama vile Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim waliojiunga na Simba.
Pia Andrew Vicent 'Dante' alishasajiliwa na mahasimu wa Simba, Dar Young Africans.
Sunday, July 17, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment