Arsenal wamefanikiwa kumnasa mshambuliaji Takuma Asano kutoka klabu ya Sanfrecce Hiroshima ya Japan
Arsenal wamethibitisha dili hilo leo na kufanikiwa kukamilisha makubaliano ya awali huku taratibu nyingine za kufanya vipimo vya afya na kusaini mkataba vikifuata".
Hata hivyo, Arsenal hawajaweka wazi ni mkataba wa muda gani wataingia na mchezaji huyo na kiasi gani atalipwa pia, huku Arsene Wenger akijinasibu kufurahishwa sana kupata saini ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 21.
Wenger amesema: "Takuma ni mchezaji kijana, mwenye kipaji kikubwa na hazina kubwa kwa siku za usoni.
"Amekuwa katika kiwango bora mno kwenye klabu yake nchini Japan na tuna hamu kubwa ya kuone akizidi kupata mafanikio hapa kadri miaka inavyozid kusonga."
0 comments:
Post a Comment