Friday, July 1, 2016

Robo fainali ya pili ya Euro mwaka 2016 inaendelea tena leo, ambapo Wales wanavaana uso kwa uso na Ubelgiji, mchezo utakaofanyika kunako uwanja wa Stade Pierre-Mauroy uliopo karibu kabisa na manispaa ya Lille majira ya saa nne za usiku.
Nahodha wa Wales Ashley Williams ambaye alikuwa na hatihati ya kuukosa mchezo wa leo kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya bega atajumuishwa katika kikosi baada ya kuwa fiti.
Beki huyo wa kati alipata maumivu hayo katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ireland ya Kaskazini wakati akishangilia goli.
Nohodha wa Ubelgiji Eden Hazard yuko fiti kwa asilimia 100 kuwakabili wapinzani wao leo baada ya hapo awali kusumbuliwa na maumivu ya paja.
Lakini Thomas Vermaelen hatakuwepo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano huku beki mwenza Jan Vertonghen akikosekana pia kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti aliyopata wakati wa mazoezi.
"Nalazimika kusema kwamba kwangu mimi michuano ya Euro ndio imeishia hapa," beki huyo wa Spurs ali-tweet, wakati huo Hazard amesema: "Nimezoea kucheza na Jan upande wa kushoto, lakini hakuna nanma itatulazimu kukabiliana na hiyo hali."
Wakati huo huo, Williams ametoa shukrani zake za dhati kwa timu ya madaktari wa Wales kufuatia kumtibitishia kuwepo katika mchezo wa leo dhidi ya Ubelgiji.
"Ni dhahiri kwamba nilijihisi vibaya sana kuumia baada ya mchezo kumalizika, lakini shukrani za kipekee ziwafikie madaktari wa timu," alisema.
"Wamefanya kazi kubwa sana kuhakikisha napona na nimefanya mazoezi vizuri kabisa na ama hakika niko fiti kabisa katika mchezo wa leo."
Kocha wa Wales Chris Coleman amesema: "Nimefarijika sana. pengine inawezekana nimepitwa na wakati, lakini unahitaji wachezaji viongozi pindi timu yako inapokuwa uwanjani.
"Timu yetu ina utulivu wa hali ya juu na hii inatokana na uongozi bora wa  Ashley. Mnapokuwa na umoja katika timu, unahitaji pia mtu makini wa kuongoza na Ash ni mtu sahihi kwa hilo."
Wachezaji wa Wales kama Ben Davies, Aaron Ramsey, Neil Taylor na Sam Vokes wote wana kadi za njano na endapo watapata tena kadi katika mchezo wa leo na kufuzu kufuzu nusu fainali, basi hawatacheza mchezo huo.
Mshambuliaji mahiri wa Wales Gareth Bale anasema kwamba, Wales wameimarika tangu kuanza kwa mashindano haya na anaamini kwamba matokeo mazuri yanawaongezea kujiamini na kuweza kuzifunga timu kubwa".
Eden Hazard kwa upande wake anasema wanahitaji kupambana kwa bidii ili kupenja ngome ya Wales katika mchezo wa leo.
Hazard alikuwemo katika mchezo ambao Wales walishinda goli moja dhidi ya Ubelgiji lililofungwa na Gareth Bale, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Cardiff City June 2015.
"Hatukuwa na mchezo mzuri kwa sababu hatukutengeneza nafasi nyingi katika mchezo dhidi ya Wales hivi karibuni," Hazard amesema.
"Tulihangaika sana kupata magoli. Wana safu ya ulinzi imara sana, nyuma kule wanasimama watu wanne na kukupa wakati mgumu sana kupenya.
"Wana wachezaji wa kiwango cha juu kabisa katika safu ya kiungo na vile vile eneo la ushambuliaji. Lakini naamini mchezo wa leo utakuwa tofauti kidogo na ule wa mwisho tuliocheza nao."
"Naamini tutatengeneza nafasi za kutosha na kufunga magoli."


Rekodi ya michezo waliyokutana
  • Ubelgiji wameshinda michezo yao mitano iliyopita kati ya 12 waliyocheza, huku Wales wakishinda mara nne na kutoka sare mara tatu.
  • Ubelgiji wameshindwa kupata goli dhidi ya Wales katika mchezo wa hatua ya kufuzu kucheza Euro mwaka, awali walitoka suluhu jijini Brussels na kufungwa 1-0 jijini Cardiff, goli lililofungwa na Gareth Bale.
  • Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana katika fainali za michuano mbalimbali mikubwa.
Wales
  • Wales hawajwahi kufika hatua ya robo fainali katika michuano yoyote mikubwa hapo kabla. Hii ni ni moja ya hatua bora kabisa kuwahi kufika tangu walipofanya hivyo kwenye Kombe la Dunia mwaka 1958 nchini Brazil na kufungwa 1-0 na Brazil.
  • Mgaoli matatu ambayo Wales wameruhusu katika michuano hii yamefungwa kuanzia dakika 56 kuendelea na yote yamefungwa na wachezaji waliotokea benchi.
  • Wales walipiga shuti moja tu lililolenga lango katika mchezo wao uliopita dhidi ya Ireland ya Kaskazini, shuti ambalo lilitokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Gareth Bale.
  • Aaron Ramsey amehusika katika magoli matatu kati ya matano ya mwisho yalifungwa na Wales (ukiondoa goli la kujifunga la Gareth McAuley wa Northern Ireland).
  • Wales wamepata 'clean sheets' mbili mfululizo kwa mara ya kwanza katika historia yao kwenye michuano mikubwa.
Ubelgiji
  • Mara ya mwisho Ubelgiji kufuka hatua ya nusu fainali katika michuano mbalimbali ilikuwa ni katika Kombe la Dunia mwaka 1986 ambapo walimaliza nafasi ya nne.
  • Magoli saba kati ya nane ya Ubelgiji katika michuano ya Euro mwaka huu yamefungwa baada ya kipindi cha kwanza
  • Kevin de Bruyne amehusika moja kwa moja katika magoli 12 kwenye michezo 12 ya Ubelgiji (magoli matao, pasi za magoli saba)
  • Hawaruhusu bao lolote katika michezo mitatu iliyopita. Ikiwa ni muda mrefu zaidi kuwahi kutokea katika historia ya timu yao kwenye michuano mikubwa.
  • Eden Hazard ametoa assist za magoli matatu katika michuano ya Euro mwaka huu, akifikia rekodi yake ya Ligi Kuu England msimu wa 2015-16
  • Hazard alifanikiwa kupiga chenga 12 dhidi ya Hungary, chenga nyingi zaid katika michuano hii tangu mwaka 1980.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video