Mshambuliaji tegemezi wa Yanga Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma amesema kwamba mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama ya Ghana ni muhimu kwao kwa ajili ya kufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua inayofuata, mchezo ambao utafanyika uwanja wa Taifa majira ya saa 10 za jioni.
Amesema wao kama wachezaji hawajisikii vizuri kutokana na timu yao kuburuza mkia katika kundi lao kufuatia kupoteza michezo yote miwili.
“Hatujafunga na hatuna pointi yoyote jambo ambalo siyo zuri kwetu, nafikiri tukifanya vizuri katika mechi ya kesho itatufanya tufufue matumaini. Tutapambana kwa muda wote,” alisema Ngoma wakati wakimaliza mazoezi ya mwisho leo kabla ya kuwakabili wapinzani wao hapo kesho.
Mpaka sasa Yanga ndio wanaburuza mkia wakiwa hawana hata alama moja nyuma ya TP Mazembe, MO Bejaia na Medeama.
0 comments:
Post a Comment