
Jose Mourinho amedai kwamba hahusiki kwa namna yoyoye ile kuondoka kwa Ryan Giggs kunako klabu ya Manchester United.
Giggs aliamua kuachana na Manchester United Jumamosi ya wiki iliyopita na kukamlisha kipindi chake cha miaka 29 ya mafanikio aliyodumu kwa miamba hao wa Old Trafford.
Insemekana kwamba, Giggs hakuridhika na unamuzi wa klabu kutompa nafasi ya kuwa meneja mkuu licha ya kumuahidi hapo awali.
"Hili sio kosa langu mimi kwa Ryan kuondoka hapa klabuni. Kazi ambayo Ryan aliitaka ndiyo hii ambayo klabu imenipa, Ryan alitaka kuwa meneja mkuu wa Manchester United manager," amesema
"Hili sio kosa langu. waliamua kunipa mimi hii kazi. Ryan aliamua kwamba anataka kuwa meneja mkuu. Mimi nilishafanya maamuzi hayo miaka takriban 14, 15 au 16 hivi iliyopita, kwamba nilitaka kuwa meneja.
"Angeweza kubaki kama angetaka kubaki klabuni hapa. Klabu ilitaka kumpa kazi yoyote nyingine hapa klabuni, lakini ameamua kufanya maamuzi ambayo yanahitaji ujasiri mkubwa."
"Si rahisi hata kidogo. Mwaka 2000 nilikuwa Barcelona na nilikuwa na mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kubaki pale kama kocha msaidizi, unadhani ilikuwa rahisi kwangu kuamua kuachana na klabu kubwa kama ile na kwenda sehemu nyingine kuanzisha mapambano mapya?
"Vivyo hivyo si rahisi kwa Ryan, na kamwe haiwezi kuwa rahisi kutoka kuwa meneja msaidizi kwenda kubeba majukumu mapya.
"Lakini namtaia kila la heri, kama siku moja atataka kurudi na kukuta bado nipo kamwe sitamzuia.
"Na kama siku moja klabu itaamua kumpa nafasi ya kuwa meneja mkuu, nadhani litakuwa ni jambo lenye mantiki kubwa, ambalo hasa linatokana na matokeo ya mafanikio aliyopata kwenye kazi yake ya umeneja."
0 comments:
Post a Comment