Sunday, July 17, 2016

Ligi ya Tanzania ilianza mwaka 1965 ikiitwa mashindano ya kutafuta klabu bingwa ya taifa, au ligi ya taifa.

Katika sehemu ya kwanza tuliona namna ambavyo mechi ya watani wa jadi, Sunderland na Yanga, ilivyoharibu msimu. 

Leo tunaangalia msimu wa pili, 1966...endelea.

Msimu wa pili wa ligi ya taifa, 1966, FAT iliongeza udadi ya timu shiriki kutoka sita za msimu wa kwanza mpaka kumi.

Africans Sports- Tanga
Coastal Union-Tanga
Cosmopolitan-Pwani
Manchester United -Tanga
Morogoro Combined-Morogoro
Sunderland -Pwani
Sunderland-Tanga
TPC-Moshi Kilimanjaro
Tobacco (Sigara) Pwani
Yanga -Pwani

Kama msimu uliotangulia, msimu huu pia ulikuwa na mikasa  tena mikubwa pengine kushinda hata ile ya msimu wa kwanza. Kwa mfano;  Africans Sports ya Tanga, moja ya timu zilizofaidika na ongezeko la idadi ya timu kwenye ligi, ilikwenda uwanjani (Municipal Stadium- siku hizi Mkwakwani) kucheza na Coastal Union lakini Coastal Union hawakutokea na ikasemekana kuwa taarifa kuahirisha mchezo ilitolewa mapema na FAT. Coastal Union walipata taarifa lakini Africans Sports hawakupata. FAT ikapanga mchezo ufanyike siku nyingine, Africans Sports wakagoma na kukata rufaa wakitaka wapewe ushindi wao. FAT ikaikataa rufani ya Sports na wao wakajibu kwa kujitoa kwenye ligi. Coastal wakapewa ushindi wa mezani.

Dar Es Salaam nako kukawaka moto. Watani wa jadi, Sunderland  na Yanga walikutana kwenye mchezo wa pili Novemba 5, 1966 (mchezo wa kwanza ulifanyika Juni 3, 1966 na Yanga kushinda 3-2. Wafungaji:
Yanga: Abdulrahman Lukongo dk. 54, Andrew Tematema dk 67, Emmanuel Makaidi dk. 83. Sunderland: Mustafa Choteka dk 24, Haji Lesso dk. 86.)

Katika mchezo huo wa pili, Yanga walikuwa wanaongoza 2-0 mpaka dakika ya 75 pale mchezaji wao mmoja alipoamriwa na refa kutoka nje ya uwanja (wakati huo kadi nyekundu zilikuwa hazijaanza kutumika duniani. Mchezaji alikuwa anaamriwa tu kutoka pasipo na kuonyeshwa kadi).

Viongozi wa Yanga walimkataza kutoka, baada ya malumbano refa akavunja pambano.

FAT wakaamua mchezo urudiwe, mchezaji aliyesababisha mgogoro afungiwe michezo mitatu na nahodha wa Yanga afungiwe miezi 12. FAT pia ikaidhabu Yanga kukosa sehemu ya mapato yake ya mchezo ule.

Uamuzi huu ukawakera Yanga, wakajitoa kwenye ligi. Mpaka wakati huo, ligi ilikuwa katika mzunguko wa 13 na Yanga walikuwa nafasi tatu na African Sports walikuwa katika nafasi ya pili.

Viongozi wa FAT na wa michezo mingine wakazisihi Yanga na African Sports kutojitoa, wakakubali na kuendelea na ligi. Hata hivyo, Yanga walikubali kurudi kwa sharti la kupewa ushindi wao na kusamehewa adhabu zote. Fat walikubali!

Mwisho wa msimu, Sunderland waliibuka mabingwa kwa kujipatia pointi 29 baada ya michezo 18. Wakipoteza miwili tu dhidi ya Yanga. Yanga walimaliza katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 22 nyuma ya African Sports iliyokuwa na pointi 25 (nafasi ya pili) na TPC pointi 24 nafasi ya tatu.

Msimamo wa mwisho ulikuwa kama ifuatavyo

                  P   W  D  L   F   A  Pts
S'land-PN  18  13  3  2  49  18  29  
A. Sports   18  11   3  4  44  18  25
TPC            18  10  4  5  44  18  22
Yanga        18  10  2  6  33  26 22
Cosmo       18   8   5  5  38  29  21
Coastal U.  18   7   3  8  32  45  17
Moro C.      18   7   3  8  35  38  17
Tobacco     18   7   3  8  28  35  17
Man. U       18   3   1  14 24  51  7
S'land-TG  18   0   1  17  15  59  1
    
Zaka Zakazi
0718171078

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video