Wapinzani wa Yanga katika Michuano ya Kombe la Shirikisho la barani Afrika (CAF Confederation Cup), Medeama S.C. ya Ghana watawasili leo majira ya saa sita mchana.
Awali Medeama walitarajiwa kufika mapema leo asubini lakini kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuwekwa wazi, wawakilishi hao pekee wa ghana katika michuano ya kimataifa watawasili mchana wa leo.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Alfred Lucas, wakali hao kutoka Ghana watawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere kwa Shirikia la Ndege la Kenya Airways (KQ) saa sita mchana wa leo, huku wakiwasili kimafungu-mafungu
0 comments:
Post a Comment