Jana Jose Mourinho alipata fursa ya kukaa kwenye benchi kwa mara ya kwanza akiwa kama kocha wa United wakati timu hiyo ilipocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wigan na kuibuka na ushindi wa magoli 2-0, magoli yaliyofungwa na Will Keane and Andreas Pereira,
Mourinho aliwatumia baadhi wa wachezaji wapya na makinda wa timu hiyo ili kuanza kufanya upembuzi yakinifu
Henrikh Mkhitaryan ambaye amesajiliwa klabuni hapo alikuwa mmoja wapo katika mchezo huo na kucheza kwa kiwango cha juu kabisa.
Baada ya mchezo huo kumalizika, Mkhitaryan alikuwa na machache ya kusema juu ya mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo mpya na kusema kwamba amefurahishwa na anaamini atazidi kuonesha uwezo wake kadri siku zitakavosonga.
Mkhitaryan alicheza dakika 45 kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Juan Mata, ambaye ana hati hati kubwa ya kuondoka klabuni hapo.
Mchezahi huyo wa kimataifa wa Armenia alichezeshwa namba kumi na alipoulizwa endapo atachezeshwa tofauti na hapo alijibu: “Haijalishi nimechezeshwa wapi iwe ama nyuma ya mshambuliaji au pembeni nitacheza kwa kiwango kile kile."
Video
Video
0 comments:
Post a Comment