Kelvin Yondani ni moja ya wachezaji waliocheza kwa kiwango cha juu kwa upande wa Yanga licha ya timu yake kushindwa kuibuka na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama ya Ghana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo wa jana Yondani alipambana vya kutisha kiasi cha mara nyingi kuonekana akipanda mbele kusukuma mashambulizi kwenye lango la timu ya Medeama licha ya juhudi zake kugonga mwamba.
Matokeo hayo ya sare hayajaonekana kumkatisha tamaa bali yamemfanya kuongeza morali na kupambana mpaka tone la mwisho katika michezo inayofuata.
Katika ukurasa wake wa Instagram Yondan ameandika hivi: "Hakuna awezae kuzuia Nguvu ya Mungu. We still fighting! And we still hope. Thanks for support. #teamyanga# @yangasc."
0 comments:
Post a Comment