Kocha wa Manchester Jose Mourinho amemuelezea kwa maneno matatu straika wake mpya Zlatan Ibrahimovic.
Mreno huyo amefanikiwa kumnasa mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan, Barcelona, AC Milan Paris Saint-Germain kwenye dirisha hili la usajili baada ya kumaliza kazi iliyompeleka nchini Ufaransa akiwa na PSG.
Wawili hao walipata wakati murua sana walipokuwa Inter Milan, na Mourinho amekanusha vikali kwamba straika huyo ni mtu mwenye maringo na majivuno makubwa.
“Nina maneno matatu tu ya kumwelezea Zlatan, ni mshindi, mfungaji hodari na vile vile ni mcheshi,” amesema Mourinho..
“Unahitaji kumwelewa kwa uzuri. Ni mcheshi sana na kama humfahamu vizuri, halafu ukasikiliza na kusoma nukuu zake basi unaweza kudhani ni mtu mwenye majivuno makubwa sana.
“Lakini ukweli ni kwamba, Zlatan ni mtu mcheshi sana. Hivyo naweza kusema kwamba, ni mcheshi, mshindi na mfungaji. Nimekuwa na furaha sana kumpata, na ni dhahiri kwamba yeye pia ana furaha kubwa kufanya kazi na mimi.”
0 comments:
Post a Comment