Manchester City wamemsajili kiungo kutoka Ukraine, Oleksander Zinchenko, 19, kutoka klabu ya FC Ufa.
Mchezaji huyo aliichezea Ukraine katika michuano ya Euro 2016, akicheza mechi zote tatu za ngazi ya makundi kabla ya kuondolewa.
Ukraine ilishindwa kufunga hata goli moja katika kundi C dhidi ya Ujerumani, Ireland ya Kaskazini na Poland.
Zinchenko anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na City chini ya meneja mpya Pep Guardiola. Wengine ni Ilkay Gundogan, Aaron Mooy na Nolito.
0 comments:
Post a Comment