Jose Mourinho kwa mara ya kwanza jana alisimama kama kocha wa Manchester United kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Wigan Wigan Athletic na kushuhudia timu yake ikipata ushindi wa mabao 2-0, magoli yaliyofungwa na Will Keane na Andreas Pereira.
Haya ndio mambo manne makubwa yalioonekana kutokana na mchezo wa jana.
1. Aina yake ya Staili ya uchezaji imeanza kuonekana
Licha ya kwamba huo ndio ulikuwa mchezo wa kwanza kama kocha wa Manchester United, lakini tayari kumeokana viashiria vya aina yake ya mchezo katika timu hiyo. Walikuwa wanamiliki mpira kidogo huku wakitumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao pia ulikuwa ukitumiwa na kocha wa zamani wa klabu hiyo Louis van Gaal lakini utofauti ulikuwepo kwenye tempo ya mchezo. Jana mchezo ulikuwa kwenye tempo ya hali ya juu. Wachezaji walikuwa na uhuru mwingi lakini vile vile aina ya mashambulizi yalikuwa ni ya moja kwa moja, na pia baadhi ya wachezaji walionekana kuwa nguvu kubwa kama Ander Herrera.
Baada ya mchezo Mourinho mwenyewe alionekana kuanza kuwakubali wachezaji wake na kusema kwamba wachezaji wanaonesha kuelewa anachowaelekeza.
2. Henrikh Mkhitaryan anaweza kuchezeshwa namba 10 ya kudumu
Watu wengi walikuwa wakitupia macho kwa wachezaji wapya hasa Henrikh Mkhitaryan. Licha ya kukosa goli la wazi lakini alionekana kuonesha uwezo wa hali ya juu. Mipira yake mingi ilionekana kuwa na hatari, alikuwa akizunguka sehemu zote za uwanja...kulia, kushoto na katikati. Ikumbukwe huyu ndiyo mchezaji aliyeongoza kwa kupiga pasi nyingi za mabao msimu uliopita kwenye ligi ya Bundesliga wakati akicheza Borussia Dortmund.
3. Luke Shaw anaonekana kumvutia bosi wake mpya.
Baada ya kukaa nje kwa miezi 10 kutokana na jeraha mguu, Luke Shaw alionekana kutokuwa na woga na kupandisha timu wakati akicheza beki ya kulia.
Zaidi ya hapo Mourinho alimsifu sana baada ya kuamua kuahirisha kwenda mapumzikoni na kuamua kufanya mazoezi kwa bidii ili kurejea katika ubora wake wa awali baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.
5. Juan Mata alikuwa na mchango mkubwa licha kuingia kipindi cha pili
Katika kikosi cha kwanza kilichotajwa katika mchezo dhidi ya Wigan hapo jana, jina la Mata halikuwepo na kwamba Mourinho alimuanzisha benchi. Katika mabadiliko aliyofanya kipindi cha pili, Mourinho alimuingiza Mata na kutoa pasi ya goli la kwanza lililofungwa na Will Keane baada ya kuunasa kwa umaridadi wa hali ya juu mpira uliokuwa ukipigwa na kipa wa Wigan kwenda kwa beki wake.
0 comments:
Post a Comment