Nahodha wa Yanga Nadiri Haroub Ali 'Cannavaro' amewaasa washabiki wa klabu hiyo kujitkeza kwa wingi kesho uwanja wa taifa kwa ajili ya kuwapa sapoti kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana, mchezo utakaopigwa majira ya saa 10 za jioni.
Nadir ametanabaisha kwamba sapoti na dua za mashabiki na Watanzania wote kwa ujumla ni ngao muhimu kwa klabu hiyo kwenye mchezo wa kesho.
"Tunamshukuru mungu tumemaliza mazoezi salama ila tu nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutushangilia kesho...tunaomba wasife moyo tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho tutapambana ila tu watuombee dua tuweze kufanya vizuri." Nadir alisema baada ya kumaliza mazoezi ya leo ambayo ni ya mwisho kuelekea kukwaana na Medeama SC hapo kesho jioni.
Yanga wapo wanaburuza mkia kwenye kundi A wakiwa hawana pointi wala goli, wakiwa nyuma ya timu vinara TP Mazembe wenye alama 6, MO Bejaia wenye alama 4 na Medeama wenye alama 1.
Yanga ndio wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye Michuano ya Afrika kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment