Paul Pogba alikuwa ni mwenye furaha kubwa baada ya ushindi kwenye nusu fainali ya Euro dhidi ya Ujerumani baada kushiriki katika upatikanaji wa goli la pili.
Lakini ilikuwa kinyume chake wakati Ufaransa ilipopoteza mchezo wa fainali dhidi ya Ureno.
Kiungo huyo wa Juventus ambaye anahusishwa kujiunga na Manchester United alionekana kutokuwa na kiwango bora katika mchezo huo.
Akiwa amechezeshwa zaidi kama kiungo mkabaji, mara nyingi Pogba alishindwa kuendana na kasi ya viungo wa Ureno na kufeli kuchukua baadhi ya mipira.
Kama hiyo haitoshi alionekana ni mtu mwenye hasira nyingi baada ya Ureno kupata goli na kuhamishia hasira hizo kwa wachezaji wenzake.
Baada ya goli hilo Pogba alionekana kuwakoromea wachezaji wenzake kama Sissoko, Matuidi na Andre-Pierre Gignac akiwatuhumu kuwa ndio sababu kubwa ya kufungwa kwao.
0 comments:
Post a Comment