Friday, July 1, 2016

Zilikuwa ni tetesi na hatimaye imethibitikia na kukamilika, ambapo Manchester United leo wamemtambulisha rasmi Zlatan Ibrahimovich kuwa mchezaji wao.
Ibrahimovich ambaye alifunga magoli mujarab 156 katika michezo 180 kunako klabu ya Paris Saint Germain, jana kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii aliweka wazi kuwa anakwenda kujiunga na Manchester United, lakini United hawakusema chochote mpaka leo walipoamua kumtangaza rasmi.
Msweden huyo anakuja United kama moja ya wachezaji wenye CV kubwa katika mchezo wa soka ulimwenguni, akiwa ameshinda ubingwa wa ligi kuu mara nne katika nchi tofauti-tofauti tangu aanze kucheza soka la kulipwa kunako klabu ya Malmo (1999). Ameifungia timu yake ya taifa magoli 62 kwenye michezo 116 na sasa aliamua kustaafu rasmi soka la kimataifa mwezi uliopita.

Zlatan amefurahia sana kujiunga na Manchester United
Zlatan amesema kwamba ana furaha kubwa ya kujiunga na United na kuwa mwenye furaha zaidi kufuatia kucheza kwa mara nyingine tena chini ya kocha wake kipenzi Jose Mourinho.
“Nina furaha kubwa kujiunga na Manchester United na nasubiri kwa hamu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya England na kucheza kwa mara ya kwanza.”  Zlatan amesema.
“Sitakuwa muungwana kama sitabainisha furaha yangu ya kuungana kwa mara nyingine tena Jose Mourinho. Ni kocha mzuri na nipo tayari kupata changamoto mpya kutoka kwake. Mara nyingi nimekuwa nikifurahia maisha yangu ya soka mpaka sasa na nina kumbukumbu nzuri nyingi sana. Na sasa nakuja England kuweka kumbukumbu nyingine tena .”

Kauli ya Jose Mourinho juu ya ujio wa Zlatan
Inavutia kwa kiasi kikubwa kuona namna gani Zlatan atatikisa kunako ligi ya England huku watu wengi wakiwa bado na kiu ya kuona ufundi wake licha ya umri wake kusonga, hata hivyo Mourinho anaamini kwamba, Msweden huyo hatakuwa na tatizo lolote na ana matarajio makubwa kwamba atafanya makubwa sana kwenye msimu ujao wa ligi na kusaidia timu yake kushinda mataji mbalimbali.

“Zlatan hahitaji utambulisho. Takwimu zinajieleza zenyewe. Ibra ni moja ya washambuliaji bora kabisa kwa sasa ulimwenguni na ni mchezaji ambaye mara zote amekuwa akijitolea kwa asilimia 100 . Amefanikiwa kushinda ubingwa muhimu wa ligi katika ulimwengu wa soka, na sasa ana fursa nyingine ya kucheza katika ligi bora kabisa ulimwenguni na naamini atatumia fursa hii kufanya kila awezalo kuisaidia timu kushinda mataji. Naamini kwamba kipaji chake kitawafa furaha kubwa mashabiki katika dimba la Old Trafford msimu ujao na uzoefu wake utakuwa na thamami kubwa katika kutoa mchango kwa wachezaji vijana katika timu,”  Mourinho amesema

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video