Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba, Ame Ali 'Zungu' ametua katika kambi ya timu hiyo iliyopo mkoani Morogoro tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.
Ame aliyesajiliwa na Simba kwa mkopo kutoka Azam FC amesema kwamba, kwa kushirikiana na wachezaji wenzake na benchi la ufundi atahakikisha anaisaidia klabu hiyo kufanya vizuri kwenye ligi na michuano mingine.
Ameongeza kwamba, yeye kama mchezaji atajituma kwa nguvu zake zote bila kujali namba atayopangiwa kucheza licha ya kukiri kwamba, angependelea zaidi kucheza kama mshambuliaji wa mwisho maana ndiyo nafasi pekee anayoimudu vyema.
"Tumuombe Mungu kwasababu kila kitu Mungu, kwahiyo tumuombe Mungu, kitakachowezekana zaidi nitakifanya, kama haitawezekana basi, lakini matarajio yangu makubwa nifanye makubwa zaidi ya yale niliyofanya pale Azam," amesema Ame.
"Aaah! sijajua, nadhani kila kitu tumuchie yeye (Kocha Omog), mimi ni straika, yeye ameona kazi yangu na ndio maana akapendekeza jina langu na naamini atanichezesha kama straika," ameongeza.
"Mimi ni Straika na nafasi yangu ndio hiyo, ila kwasababu mchagua jembe sio mkulima, popote nitakapowekwa nitacheza."
0 comments:
Post a Comment