Klabu ya Manchester United imetanabaisha kwamba tayari mchezaji wao mpya Zlatan Ibrahimovic amevunja rekodi ya kuwa na nguvu nyingi wakati akifanyiwa vipimo vya afya baada ya kukamilisha uhamisho wake kujiunga na wakali hao wa Old Trafford.
Zlatan (34) ambaye mkataba wake na Paris Saint-Germain ulimalizika mwezi June mwaka huu alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu kuungana na Jose Mourinho kunako klabu ya United.
Ibrahimovic alithibitisha uhamisho wake kuelekea klabu ya Man United kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram Ijumaa kwa namna yake hata kablya ya klabu yenyewe kutoa taarifa rasmi.
Kikubwa ilichowashtua watu wengi ni kwamba, nahodha huyo wa zamani wa Sweden tayari ameshavunja rekodi kabla hata ya kusaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo.
Hata hivyo, United hawajoa taarifa zozote kwa undani juu ya rekodi hiyo, lakini Zlatan tayari ameanza kuacha alama klabuni hapa.
0 comments:
Post a Comment