Bastian Schweinsteiger hakucheza kutokana na taarifa zilizoenea kueleza kwamba, Mourinho amedai hayupo kwenye mipango yake.
"Kama wachezaji hawakuwa kwenye mipango yangu, nisingeweza kuwapa hata dakika moja. Nisingeweza pia kuwajumuisha kwenye kikosi changu
"Kikosi kina ushindani mkubwa, kina umuhimu mkubwa kuelekea msimu mpya.
"Tuna michezo 38 kwenye ligi ya Englanda, tuna uwezekano wa kuwa na michezo 15 katika mashindano ya Europa, jumlisha na makombe ya ndani, tutakuwa na takriban michezo 60. Hivyo kwa idadi hiyo ya mechi hatuwezi kufanikiwa kwa kuchezesha wachezaji 11 tu.
"Unapokuwa kikosini unatakwa kutambua kwamba, kikosi ni muhimu zaidi kuliko mchezaji mmoja-mmoja, klabu ni muhimu kuliko sisi sote, na ili kuwa kwenye kikosi lazima uwe tayari kwa haya yote, kucheza ama kutocheza, kucheza sana, kucheza mara cheche, kucheza dakika moja, kutokuchaguliwa. Kila kitu ni sehemu ya maisha ya kikosi hiki."
0 comments:
Post a Comment