Monday, July 4, 2016

Kocha wa timu Ujerumani Joachim Low, ambaye timu yake itakumbana na Ufaransa kwenye mchezo wa nusu fainali ya Euro mwaka huu amesikitishwa na kukosekana kwa mshambuliaji wake Mario Gomez ambaye anasumbuliwa na jeraha la misuli ya paja.
Pia kuna uwezekano mkubwa wa kuwakosa Sami Khedira na Bastian Schweinsteiger ambao wanasumbuliwa pia na majeraha tofauti-tofauti.
Low amesema: "Inauma sana kuwakosa wachezaji muhimu, hasa katika hatua nyeti kama hii."
Gomez, ambaye ni mshambuliaji pekee wa Ujerumani anayetambulika kwenye michuano hii, alitolewa katika kipindi cha pili kwenye mchezo wa Jumapili na alihusika pia katika goli la Ozil lililowekwa kimiani dakika ya 65.
"Natoa pole zangu za dhati kwa Mario. Amefanya kazi kubwa sana katika michuano ya mwaka huu na kuisaidia sana timu, si tu kwa magoli yake bali mchezo mzima kwa ujumla," Low aliongeza.
"Hii ina maana kwamba tunatakiwa kukubaliana na hali halisi na kuitafutia ufumbuzi mara moja. Na naamini tutafanya hivyo."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video