Wednesday, July 13, 2016

Hivi karibuni Kamati ya Nidhamu na Maadili ya TFF ilitangaza kumfungia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga Jerry Cornel Muro kujishughulisha na masuala ya soka nchini kwa mwaka mmoja kutokana na kile kinachodaiwa kutoa kauli zisizo na nidhamu kwa shirikikisho hilo.
Baada ya taarifa hiyo kumfikia Muro ambaye alikuwa mapumzikoni mjini Moshi alisema angepambana nao punde tu atakaporejea jijini Dar es Salaa.
Lakini leo hii kupitia akaunti yake ya Instagram, Muro ameandika maneno yenye kuashrikia kunyanyua mikoano juu na kukubali adhabu hiyo ya kifungo aliyopewa.
Ameandika hivi: "Kila nikizifikiria figisu za soka la bonge aisee nachoka kabisaa, let me walk away for a while though I will be missing my funs and my people wa kimataifa but I must walk away for a while @yangasc."


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video