Winga wa Yanga Simon Msuva anaamini klabu yake bado inanafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya nufu fainali ya kombe la shirikisho Afrika licha ya kuwa na pointi moja pekee kwenye Kundi A linaloongozwa na TP Mazembe yenye pointi sita ikiwa bado haijacheza mechi yake ya tatu dhidi ya MO Bejaia.
Msuva ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya mchezo wa Yanga na Medeama kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wa taifa huku timu yake ikipata pointi ya kwanza baada ya kushuka uwanjani mara tatu.
“Kwa upande wetu matokeo sio mazuri, ukizingatia tulikuwa nyumbani na mashabiki walijitokeza kwa wingi wakiwa na imani kwamba timu itafanya vizuri lakini hata haya matokeo siyo mabaya kama wao wameweza kurudisha goli kwetu hata sisi tunauwezo wa kufanya chochote kwao kwasababu bado hatujamaliza na haya mashindano mimi naamini bado tuna nafasi,” . Msuva aliiambia shaffihdauda.co.tz
“Nafasi ipo kwasababu wapinzani wetu wengine nao wanacheza mechi zao, TP Mazembe pia hatuwezi kujua matokeo yao yatakavyokuwa lakini sisi hatuangalii sana matokeo yao sisi tunaangalia tufanye nini kwenye mechi zijazo”.
“Mashabiki wasife moyo kwasababu kwasababu timu bado nzuri inanguvu, wao wazidi kuipa support, tunaposhinda tunashinda wote na tunapofungwa tunafungwa wote,” Msuva hakuacha kuwapa moyo mashabiki wa Yanga na akitaka waungane pamoja na timu yao hadi dakika ya mwisho.
0 comments:
Post a Comment