Kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kiliketi jana Julai 2, 2016 na kupitia malalamiko ya TFF dhidi ya
- Nassib Mabrouk - Katibu wa MZFA na Msimamizi msaidizi wa kituo cha Mwanza.
- Mbasha Matutu - Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga).
- Jerry Muro, Ofisa Habari wa Young Africans S.CShauri dhidi ya Mabrouk lilisikilizwa. Lakini mashauri dhidi ya Jerry Murro na Mbasha Matutu, yaliahirishwa hadi wiki ijayo ili walalamikiwa wapate muda wa kupitia mashtaka na pia TFF kupata fursa ya kuleta mashahidi wake.TFF inatoa tahadhari kwa walalamikiwa kuacha kutumia mitandao ya kijamii kupotosha umma wakati huu mashauri yao yakiendelea kusikilizwa
0 comments:
Post a Comment