Wanachama wengi waliojitokeza walionekana kuwa na jamb moja tu wakisisitiza agenda kuu kuwa mabadiliko ya mfumo wa umiliki wa klabu kutoka uanachama wa kawaida kwenda kwenye mfumo wa hisa.
Rais wa Simba alisema uongozi uliteua kamati kkusanya maoni kwa wadau, wanachama na wapenzi kuhusu suala la mfumo wa hisa.
Kamati hio ilitoa mapendekezo ya awali ya kutaka mfumo wa hisa lakini imeomba muda zaidi kutoa ripoti na mapendekezo ya mwisho.
Hata hivyo wanachama walipinga kwa sauti na kudai muda waliopewa umetosha na wanataka mabadiliko tu.
Mkutano ulimalizika kwa mwenyekiti wa kamati ya maoni kushindwa kuendelea baada ya wanachama kuingilia hotuba yake na hivyo kumlazimu Rais Evans Aveva kusimama na kumaliza mkutano kwa staili ya pekee.
Kilichoonekana ni uongozi kukubali agenda ya mabadiliko lakini wanasubiri ripoti ya mwisho ya kamati iliyoteuliwa kukusanya maoni ya suala la mfumo wa hisa.
Credit: Soka 360
0 comments:
Post a Comment