Thursday, July 21, 2016

Mechi ya kwanza ya Pep Guardiola ya kabla ya kuanza kwa msimu imemalizika kwa Manchester City kupoteza dhidi ya klabu yake ya zamani Bayern Munich 1-0. 
Goli pekee la Bayern katika mchezo huo wa kirafiki limefungwa na Erdal Ozturk na kumpa ushindi meneja mpya Carlo Ancelotti. 
Bayern na City zote hazikuwa na wachezaji wake wa kikosi cha kwanza baada ya michuano ya Euro 2016 na Copa America, na Guardiola alikuwa na wachezaji 12 chipukizi katika kikosi chake. 
Usajili mpya Oleksandr Zinchenko alicheza kipindi cha kwanza, lakini Ilkay Gundogan na Nolito hawakuwepo. 
City sasa wanaelekea China ambapo watakutana na Manchester United siku ya Jumatatu. Kikosi kitakachosafiri kitakuwa na Sergio Aguero, David Silva, Nolito, Raheem Sterling na Joe Hart.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video