Pep Guardiola amekuja England kuthibitisha uwezo wake baada ya kufanya hivyo nchini ya Uhispania na Ujerumani
Jumapili alitambulishwa kwa mashabiki na kuonesha shauku yake ya kuwafahamu wachezaji wake kwa undani. Na Jumatatu kwenye mahojiano yake na mwandishi Noel Gallagher, alisema kwamba amekuja hapa kuthibitisha uwezo wake kwa watu wote wenye mashaka juu ya ubora wake, lakini kwa mikakati maalum ya kupambana na aina ya soka la England ambalo linasifika kwa matumizi ya nguvu.
Jana Ijumaa aliitisha mkutano mkubwa na waandishi wa habari na kuelezea nia yake ya kufanya maajabu katika soka la England.
Lakini hajaonekana kuahidi mabadiliko ya ghafla kwa aina ya soka ambalo anapenda kufundisha, soka la pasi nyingi.
Miaka nane iliyopita alipata nafasi ya kuifundisha Barcelona kwa mara ya kwanza akiwa bado hana uzoefu mkubwa baada ya kufundisha kwa mwaka mmoja tu ligi daraja la tatu Uhispania. Aliahidi kwamba baada ya miezi mitatu wale wote waliokuwa na shaka juu ya uzoefu wake wangebadilika na kukubali uwezo wake.
Miaka mitatu iliyopita alipotua Bayern Minich hakutoa maneno ya yenye ahadi kubwa, alikuwa mpole kabisa huku akisema "Nimekubali changamoto hii kubwa bila shaka yoyote ile. Na ndiyo maana mimi ni kocha.."
Safari hii, amekuwa muwazi kabisa. Pengine angekuwa kocha mwenye CV ndogo watu wangeshindwa kumwamini. Lakini kwa kuwa ameshafanya mambo mazito kwenye klabu mbili kubwa duniani za Barcelona na Bayern, basi watu hawawezi kuwa na shaka juu ya uwezo wake.
Wakati huo huo Mourinho ambaye ametoka mapumzikoni baada ya kutimuliwa Chelsea mwaka jana, janga ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika kazi yake ya ukocha, Jumanne alikaa mbele ya waandishi na kuwaleza kuwa yeye ndiye mtu sahihi wa kuirudisha United kwenye ubora wake, lakini Guardiola amekuwa ni mpole na asiye na ahadi nyingi safari hii.
"Ndio maana niko hapa," Guardiola alisema wakati akirejea kauli yake aliyoitoa waiki iliyopita. "Kuthibitisha uwezo wangu. Nilikuwa Barcelona ambapo nilikuwa na kila kitu, mchezaji bora kuwahi kutokea na timu ambayo wachezaji wake wengi walitokea kwenye akademi, hivyo niliifahamu vyema.
"Nimekuwa Bayern Munich, klabu ambayo ina uzoefu mkubwa vile vile vitu vingi. Huu ni mtihani mwingine kwenye kazi yangu ya ukocha. Ningekuwa na amani zaidi kuendelea kubaki mahali nilipokuwa, lakini nadhani huu ni wakati muafaka wa kuja hapa na kuonesha uwezo wangu. Kama nina uwezo wa kushawishi wachezaji hawa kwa namna ninavyotaka na kuonesha kiwango kinachostahili nasi mwisho wa siku tutaona."
Mbali na maneno yote aliyozungumza. Lakini kikubwa alichosisitiza kwake ni kulipa thamani kubwa soka la vijana kwenye timu. Vile vile kuwataka wachezaji kujituma na kuachana na mambo ya kutegemea kucheza mpira wa mdomoni (mind games).
Mourinho kwa upande wake, alisema kwamba hana nia yoyote ya kupambana na mpinzani wake huyo wa zamani. Huo pia ulikuwa msimamo wa Guardiola ambaye alifurahishwa sana na kauli hiyo: "Nadhani Jose ameongea vyema sana. Hii sio vita kati yangu na yeye."
Hajaongelea chochote kuhusu usajili mpya na suala lolote juu ya mchezaji anayempenda. Wakati anaenda Barca alitanabaisha kukunwa na uwezo wa Ronaldinho.
Samahani, nadhani hii sio sehemu sahihi ya kuelezea juu ya usajili mpya," amesema. Kwa kuheshimu wachezaji wangu, klabu nyingine, lakini mwa muda mfupi tu tayari ni kwa namna gani waandishi wa England wako vizuri na naamini mtaweza kugundua nani tunamtaka kwa sasa na nini tunataka kuelekea msimu ujao. Tunataka kujaribu kufanya mabadiliko machache, na nadhani tutafanya hivyo."
Wachezaji ambao mpaka sasa Pep amekuwa akihusishwa nao ni pamoja na ohn Stones na Leroy Sane ambao wanadaiwa kukaribia kujiunga hivi karibuni, Bruno Peres wa Torino na Leonardo Bonucci nao wako kwenye rada huku Toni Kroos na Thiago Alcantara wakiwindwa vikali pia.
Pamoja na yote hayo Guardiola bado ameonesha kusita kutoa ahadi ya mafanikio ya moja kwa moja licha ya kusisitiza kwamba amekuja kuwathibitishia wabaya wake ubora wake kwenye ligi ya England.
0 comments:
Post a Comment