Wednesday, July 20, 2016

Didier Drogba amesema kwamba Cristiano Ronaldo ambaye amempachika jina la "real leader" ndiye anapaswa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia 'Ballon d'Or' mwaka 2016 kutokana na mchango wake mkubwa kunako klabu ya Real Madrid na timu yake ya taifa ya Ureno.
Ronaldo ambaye ni mshindi wa tuzo hiyo mara tatu, ndiyo anapewa nafasi kubwa ya kuchukua tuzo hiyo mwaka huu kutokana na kutoa mchango mkubwa kwa Real Madrid kuchukua taji la UEFA na Ureno kuchukua taji la Euro huku akimwacha mpinzani wake mkubwa Messi ambaye alishindwa kuipa Argentina taji la Copa America na kuipa Barcelona ubingwa wa La Liga na Kombe la Mfalme tu.
Wachezaji wengine wanaotarajiwa kumpa changamoto kubwa Ronaldo ni pamoja na Luis Suarez na Neymar wa Barcelona, na mshambulizi fundi wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann.
"Nimecheza dhidi ya Ronaldo kwenye fainali ya Uefa mwaka 2008 ambapo Man United walishinda, Drogba aliiambia Madrid TV. "Ni kiongozi halisi na anastahili kushinda tuzo ya Ballon d'Or kutokana na kiwango bora alichokionesha Real Madrid na Ureno. Licha kwamba kwenye fainali ya Euro dhidi ya Ufaransa alitoka mapema, lakini mchango wake ulichangia kuwapa taji Ureno."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video