
Chelsea imetangaza kumsajili mshambuliaji kutoka Ubelgiji Michy Batshuayi, 22, aliyekuwa akiichezea Marseille.
Kwa mujibu wa tovuti ya Chelsea, mchezaji huyu amesaini mkataba wa miaka mitano.
Batshuayi amesema: "Nimefurahi kusaini katika moja ya klabu kubwa Ulaya na kufungua ukurasa mpya katika uchezaji wangu. Ni matumaini yangu kuwa nitaisaidia Chelsea kushinda makombe mengi nikiwa Darajani".
0 comments:
Post a Comment