Henrikh Mkhitaryan alijiunga na Borussia Dortmund mwaka 2013 akitokea klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Manchester United wamefanikiwa kumnasa nyota wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan.
Nahodha huyo wa Armenia, ambaye aliigahrimu Borussia ada ya Euro milioni 23.5 kupata saini yake, mkataba wake ulikuwa umalizike msimu ujao wa ligi.
"Kama tungesema tukatae ofa hii, mchezaji huyu angeondoka bure msimu wa mwaka 2017," mtendaji mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke aliiambia tovuti ya klabu.
Mkhitaryan, 27, bado hajafanyiwa vipimo vya afya kunako klabu ya Manchester United mpaka pale masuala yote ya kimikataba yatakapowekwa sawa.
Kama dili hili litakamilika basi atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na United kwenye dirisha hili la usajili baada ya beki Muivory Coast Eric Bailly na mshambuliaji wa zamani wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kukamilisha usajili wao.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp wakati huo akiwa Borussia ndiye aliyemsajili Mkhitaryan kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Mkhitaryan alipata tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga msimu wa 2015-16 baada ya kufunga magoli 18 kwenye michuano yote, ikiwemo katika dhidi ya Liverpool kwenye kombe la Europa mchezo uliofanyika Anfield.
Mkhitaryan ni mtoto wa mchezaji maarufu wa zamani wa Armenia, Hamlet Mkhitaryan. Alitimiza mechi 59 kwa taifa lake kabla ya kufikisha miaka 18.
0 comments:
Post a Comment