
Bale v Ronaldo
Gareth Bale jana aliongea na vyombo vya habari, kuelekea mandalizi ya mchezo wao wa nusu fainali ya Euro dhidi ya Ureno.
Kwa namna yoyote ile, mchezo huu unavuta hisia za watu wengi kutokana na uwepo wa Gareth Bale na Ronaldo, kama wachezaji wanaocheza klabu moja ya Real Madrid ambapo kwa mara ya kwanza wanakutana. lakini safari hii kila mtu akiwa kwenye timu yake ya taifa.
Kikubwa Bale amekataa kusema chochote dhidi ya Ronaldo na kusisitiz akwamba mchezo huu ni kati ya Wales na Ureno na sio Bake na Ronaldo.
Hawajatumiana ujumbe wowote wa kutakiana heri.
Bale amesema kuelekea mchezo wao wa nusu fainali wawili hao hawajatumiana hata ujumbe wa kutakiana kila la heri kwenye mchezo wa nusu fainali pindi tu timu zao zilipofuzu.
Alipouliza juu ya suala la Ronaldo kutupa Microphone za moja ya waandishi wa habari nchini Ufaransa, Bale alikataa kabisa kuzungumzia suala hilo.
0 comments:
Post a Comment