Friday, July 22, 2016

Imekuwa ni kawaida kwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger kujikongoja kama kobe kwenye madirisha mbalimbali ya usajili huku wapinzani wake wakiwa 'serious' na kazi, wakiwa na nia ya dhati kabisa ya kupata watu sahihi wa kuwapa mataji mablimbali.

Ni mwaka mwingine tena huu, tumeona dirisha liko wazi na kila timu inapambana kivyake-vyake. Tumeona Man United tayari wanao Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan huku wakijiandaa kuvunja rekodi ya usajili ulimwenguni kwa kumnasa Paul Pogba ambaye thamani yake inatajwa kuwa paundi milioni 100.

Chelsea kwa upande wao tayari wana Michy Batshuayi na N'Golo Kante ambao wote kwa pamoja thamani yao ni paundi milioni 63. Liverpool tayari wameshawanyaka watano akiwemo Msenegali kutoka Southampton Sadio Mane aliyesajiliwa kwa paundi milioni 35. Manchester City hapana shaka yoyote wako kwenye mawindo makali, na tayari mpaka sasa wameshawasajili Ikay Gundogan, kwa paundi milioni 21 na Nolito kwa paundi milioni 13.

Na kwa upande wa Washika Mtutu wa London sasa Arsenal. Tangu usajili wao wa mwanzo kabisa wa Mswisi Granit Xhaka kutoka Borussia Monchengladbach kwa ada ya paundi milioni 35 huku wakimkosa Jamie Vardy ambaye aliamua kubaki Leicester baada ya kuongeza mkataba huku wakimsajili Mjapan Asano Takuma.

Wamekuwa kama hawapo vile ama wanaogopa kupambana katika soko la usajili, ni kama wabishi vile kutafuta mchezaji mwingine baada ya Xhaka. Tayari mashabiki wa Arsenal wameshakuwa na hofu wakiamini kwamba mwaka mwingine wa kutoka kapa unakuja hasa wakiangalia usajili uliofanywa na wapinzani wao ambao ndio wanapambana nao kwa kiasi kikubwa kwenye mbio za ubingwa. Ikumbukwe tu mwaka jana Arsenal walimsajili Petr Cech tu na kutosajili mchezaji yeyote wa ndani. 

Walijaribu kutaka kumsajili Vardy baada ya kufikia kiasi cha pesa alichokuwa akiuzwa ambacho ni paundi milioni 20, lakini Vardy aliamua kubaki baada ya kukosa uhakika wa kucheza endapo angeamua kujiunga na timu hiyo.

Katika wiki za hivi karibuni, walishindwa kufanya usajili wa mchezaji muhimu sana na hatimaye Monaco kuwapiga bao. Monaco walimsajili mchezaji kutoka Lille Mfaransa Djibril Sidibe, 23, kwa ada ya euro ml 15 baada ya Arsenal kuchelewa kukataa kutoa zaidi ya kiasi kilichofikiwa makubaliano na klabu hiyo.

Beki wa kati wa Club Brugge Bjorn Engels, ambaye anatajwa kuwa zao la baadaye la Ubelgiji, bado hajasaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo. Ni mchezaji ambaye staili yake ya uchezaji inafanana kwa kiasi kikubwa na beki wa Everton anayezitoa timu nyingi udenda, pia Arsenal wanasita kuweka mikono  yao pale.

Wanaendelea na ubishi wao, huku Wenger ndio akiwa na maamuzi yote akiratibiwa kwa karibu bosi wake Stan Kroenke

Mwezi March, klabu hiyo ilianika mapato yake na kusema kuwa kuna hazina ya paundi milioni 159, kiasi ambacho kilikuwa kikubwa zaidi ya klabu yoyote ile. Baadaye wakajazwa tena noti zinazotokana na haki ya kurusha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) kiasi cha paundi bil 8.3. Ndani ya fesha hizo ni kiasi cha paundi mil 15 tu ndio zilizotumika baada ya kufanya usajili wa wachezaji wawili ambao ni Mohamed Elneny na Petr Cech. 

Pesa aliyosajiliwa Xhaka inawezekana ikawa ni kubwa lakini ukilinganisha nna hali halisi ya sasa na vilabu vingine vinavyotumia pesa ama hakika Arsenal wana kila sababu ya kujitutumua kuendelea kuimarisha kikosi chao. 

Ikumbukwe tu usajili wa Cech mwaka jana, wengi walidhani Arsenal wangendokana na jinamizi la ubingwa wa EPL tangu mara ya mwisho walivyochukua mwaka 2004, lakini badala yake wakendelea kuandamwa na tatizo kubwa la ukosefu wa uimara katika safu ya ulinzi na udhifu mkubwa wa safu ya ushambuliaji. Walimaliza nafasi ya pili nyuma ya Leicester lakini wakiachwa kwa pointi 10. attack.

Kumtegemea Giroud na sawa na kumtegemea mgonjwa akufanyie kazi, licha ya kufanya vizurio kwenye Michuano ya Euro mwaka huu, lakini angalia alichokifanya kwenye mchezo wa fainali. Alikuwa na kiwango cha ovyo kabisa na kuigharimu timu yake kukosa ndoo hiyo ambayo walikuwa wakiipagania wakiwa nyumbani. Anakosa wepesei, kasi na kuendana na mikiki-mikiki ya EPL jambo ambalo washambuliaji kama Vardy sio tatizo kwao. Danny Welbeck atakosekana mpaka mwaka 2017 licha kwamba hata yeye pia sio mshambuliaji mwenye makali kwa kiasi hicho.

Wiki iliyopita Arsenal walihusishwa na mshambulizi wa Inter Milan Mauro Icardi. Hata hivyo zoezi hilo linaweza kuwa gumu kwa Arsenal kutokana na gharama za mchezaji huyo kuwa juu. Inaarifiwa kwamba ada yake ya usajili inagharimu kiasi cha paundi mil 40, pesa ambayo kwa Arsene Wenger haitakuwa kazi rahisi kutoa ukizingatia kwamba Atletico Madrid na Juventus nao wanamtolea macho.

Bado ukuta wake hauko timamu chini ya Laurent Koscielny, Per Mertesacker na Gabriel ambapo wote kwa pamoja wanahitaji kupata mtu ambaye atawapa changamoto ya kuendana na kasi ya EPL. Mertesacker umri umemtupa mkono na hana kasi uwanjani na kwa kipute cha EPL, basi sioni akifanya maajabu yoyote.

Tumeshuhidia Wenger akifanya usajili wa panic katika siku za mwisho baada ya kufanya hivyo kwa Mesut Ozil na Danny Welbeck mwaka 2013 na 2014 mtawalia. Pengine anaweza kuwa na mpango huo huo mwaka huu pia. Lakini kama itakuwa vinginevyo sioni Arsenal kama itakuwa ni timu ya ushindani msimu ujao na hata hiyo nne bora pengine wanaweza kuisikia kwenye bomba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video