Mapema kabla ya Michuao ya Euro kuanza, Arsenal walionesha nia ya kumsajili Jamie Vardy kutoka Leicester City kabla ya kuamua kubaki klabuni hapo baada ya kuongezewa mkataba mnono.
Ilionekana kana kwamba kikoisi cha Leicester City kingeendelea kubaki kama kilivyokua msimu uliopita baada ya maamuzi hayo ya Vardy. Hata hivyo baadaye Chelsea wakaonesha nia ya kumtaka N’Golo Kante na jana wamefanikiwa kumsajili. Hili ni pigo kubwa kwa Vardy na Leicester kwani Kante alikuwa mchano mkubwa kwa mafanikio ya timu msimu uliopita.
Na taarifa nyingine zilizoenea kwenye mitandao mbali zinadai kwamba Riyad Mahrez pia anawindwa vikali na Barcelona.
Sasa baada ya matukio yote haya, mshabiki wa Arsenal wametikisa mitandaoni hasa kwenye mtandao wa Twitter wote wakimponda Vardy kukataa kujiunga na timu yao na kuamua kubaki Leicester huku wenzake wakionekana kuondoka mmoja-mmoja.
Soma Tweet hapo chini.
0 comments:
Post a Comment