Sam Allardyce ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Engand, hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Chama Cha Soka England (FA).
Allardyce (61) amechukua jukumu la kuinoa timu hiyo maarufu kama 'Three Lions' kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Roy Hodgson baada ya kutolewa na Iceland katika Michuano ya Euro mwaka huu iliyomalizika hivi karibuni nchini Ufaransa.
Allardyce amepata nafasi baada ya kumshinda kocha wa Hull City Steve Bruce na kocha wa Marekani Jurgen Klinsmann
Kocha huyo wa zamani wa Bolton Wanderers, Blackburn Rovers na West Ham United ameacha kazi kwenye klabu ya Sunderland kufuatia ya kuinusuru kutoshuka daraja msimu uliopita baada ya kudumu kalbuni hapo kwa miezi tisa tu. Amefurahia sana uteuzi huo na kusema kwamba "Sasa ni muda wa kutoa kile alichonacho".
"Nimefurahi sana kuteuliwa kuwa kocha wa England hasa kutokana na ukweli kwamba bila ya kuificha hii ni kazi ambayo kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiihitaji. Kwangu mimi, hii ni kazi bora kabisa kwenye tasnia ya soka nchini England." aliiambia tovuti ya FA.
"Nitafanya kila liwezekanalo ili kuisaidia England kufanya vizuri na kuwapa furaha mashabiki wetu, na zaidi ya yote ni kuwafanya wajivunie utaifa wao."
"Wakati mawazo yangu yote yatakuwa kwenye timu ya wakubwa na kupata matokeo mazuri, nataka niongeze ushawishi wangu mpaka kwenye timu za vijana."
Najua tuna vipaji vingi, tuna wachezaji ambao wana moyo wa dhati wa kulitumikia taifa lao na sasa ni muda muafaka wa kuwapa mashabiki wetu furaha.
Mtihani wa kwanza wa Allardyce utakuwa ni Septemba 4 wakati England watakapovaana na Slovakia.
0 comments:
Post a Comment