Thursday, June 23, 2016

Unapozungumzia moja ya washambuliaji wa kati bora na waliokamilika kuwahi kutokea ulimwenguni, basi jina la Zlatan huwezi kukosa kuliweka, na kama utakosa kufanya hivyo ama hakika utakuwa umefanya makosa makubwa sana.
Zlatan ni mshambuliaji wa ajabu, mshambuliaji ambaye mambo anayofanya hayaendani na umbo lake. Ana kila 95 na urefu wa futi 6.5, kitu ambacho ni nadra kutokea mchezaji mwenye aina ya uzito na urefu kama wake kuwa na uwezo wa kunyumbulika kama yeye. Zlatan ana kasi, anapiga chenga, mashuti, vichwa. Tumewaona wachezaji wenye urefu kama wake lakini hawana flexibility kama yeye.
Unawatazama wachezaji kama Peter Crouch (futi 6.7, kilo 75) au Per Mertesacker (futi 6.6, kila 90) unaona kabisa licha ya kuwa wamemzidi kidogo urefu lakini wao kuzidiwa uzito, hawana uwezo wa kunyumbulika kama Zlatan.
Unakumbuka goli lake la 'bicycle kick/overhead kick' dhidi ya England katika mchezo wa kirafiki ulipigwa Novemba 15 2012 katika dimba la Friends Arena?, huyo ndiyo Zlatan halisi...nani ,mwenye umbo kama lake anaweza kufunga goli kama lile? pengine yupo ila bado sijamfahamu.
Na unajua alisemaje alipoulizwa kama lile ndio goli bora kabisa katika maisha yake ya soka....alijibu: "Hapana ila ni goli ambalo linaingia kweye magoli ambayo nimewahi kuyapenda tu".
Wakati huo huo Steven Gerrard akisema: "Wakati mwingine unatakiwa kukubali uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, na hivyo ndivyo unavyoweza kusema, lilikuwa goli la kiwango cha juu kutoka kwa mchezaji wa kiwango cha dunia. Lilikuwa ni goli bora ambalo sijawahi kuliona."
Ukiachana uwezo wake ndani ya uwanja, nje ya uwanja anajiamini kupita kiasi, anaweza kujibu chochote anachojisikia. Huyu ndiyo Zltan bwana!!!!
Kama ilivyo kwa binadamu yeyote mwenye mapenzi na mchezo wa mpira wa miguu. Zlatan alianza kupenda soka la kimataifa mwaka 1994 wakati alipokuwa akiangalia timu yake ya taifa ikicheza na Brazil katika nusu fainali ya Kombe la Dunia. Kati ya Wa-sweden wote waliokuwepo uwanjani hapo, Zlatan pekee alikuwa akiishangilia Brazil badala ya Sweden. Si kana kwamba alikuwa hapendi taifa lae ila ni kwasababu Sweden ilikuwa ikicheza na Brazil.
Anasema: "Sikuwahi kuingalia Sweden ndiyo sababu kubwa, lakini niliipenda Brazil kwa sababu ilikuwa ni timu yenye utofauti mkubwa".
Baba yake alikuwa ni muislam mwenye asili ya Bosnia na mama yake mkristo wa dhehebu la Catholic katika mji wa Malmo, hivyo hakuwa na mapenzi ya dhati na Sweden kwa kuwa alihisi na Sweden haimtaki...lakini kilichotoea sasa ni kesi tofauti kabisa.
Lakini baada ya kukua na kugundua kuwa ana umuhimu gani kwa taifa hilo, Zlatan alibadilika kabisa. Kocha wa Sweden wakati huo Erik Hamren alimwita kwenye kikosi chake na kumpa moja kwa moja unahodha kwenye kikosi chake kutokana na karisma yake kubwa aliyonayo.
Maamuzi hayo yalikosolewa na Wa-sweden wengi na kusema kuwa Zlatan hakuwa amefanya chochote na hakustahili heshima hiyo.
Baada ya muda mfupi aliwafunga mdomo wote baada ya kiwango chake kikubwa na moyo wake wa dhati wa kujitolea kwa taifa hilo. Akawa kiongozi wa kweli ndani na nje ya uwanja. Ilikuwa alamanusra awapeleka Brazil mwaka 2014 lakini bahati haikuwa yao baada ya kutolewa kwenye play-off na Ureno ambapo Ronaldo aliibuka shujaa.
Alisema hivi baada ya kutolewa: "Kitu kimoja cha msingi nataka kusema, Kombe la Dunia bila ya Zlatan halitakuwa na thamani yoyote kuangalia." Pengine hiyo ilikuwa ni aina ya uchombezaji tu ila maana yake kubwa ni kwamba michuano hiyo isingekuwa na msisimko bila ya uwepo wa Zlatan.
Hata hivyo watu wengi walifurahi kuona Zlatan ameipeleka Sweden kwenye michuano ya Euro mwaka huu baada ya kuing'oa Denmark kwenye mchezo wa mtoano Novemba mwaka jana kwa wastani wa magoli 3-2.
Kwenye michuano ya Euro wakapangwa kwenye kundi lenye timu za Ubelgiji, Italy na Jamhuri ya Ireland . Ni kundi gumu lakini Wa-sweden waliamini uwepo wa Zlatan ungewapa nuru na maihs ya soka ya Zlatan kuisha kwa furaha furaha ya aina yake. Lakin badala yake imekuwa vinginevyo hatuajamuona Zlatan yule wa goli dhidi ya England na Italy ambaye magoli yake yanahitaji 'slow motion' kuyaangalia vizuri.
Kipa wa Italy Gianluigi Buffon wiki iliyopia alisema, magoli hayo yamekuwa kama desturi kwa Zltan. Aliyafanya kuoneka ya kawaida. Alifanya visivyowezekana kuwezekana. Mashabiki wa Sweden walimpenda lakini zaidi walimkubali kwa namna ambavyo aliwaongoza na namna ambavyo alikuwa akicheza ndivyo walivyozidi kumwimbia.
Walifanya tena hivyo jana kwenye mchezo wa kumaliza makundi wa kundi A dhidi ya Ubelgiji ambapo haukuisha vizuri kwa Zlatan kama namna ilivyopaswa...kwasababu ni mchezo ambao ulikuwa wa kumuaga rasmi kutokana na kutangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa. Alifunga goli katika mchezo huo lakini lilikataliwa kutokana na kufanyika madhambi kabla ya goli hilo na baadaye Radja Nainggolan kuifungia goli Ubelgiji na kuzima kabisa ndoto za Zlatan.
Katika kuzungumzia juu ya kuondoshwa kwenye michuano hii, Zlatan alisema kwamba ameseikitishwa na kiwango chake kutokuwa kizuri katika michuano hii, lakini kitu kizuri kwake ni kuwa mfungaji wa muda waote wa taifa hilo.
"Katika maisha yangu hakuna kitu kinachoitwa fedheha, bali fahari na furaha tu," amesema Zlatan. Mimi kijana kutoka eneo dogo la Malmo na kupata fursa ya kuiwakilisha nchi yangu. nimeweza kuwa nahodha...ni jambo la kujivunia.
"Najivunia mafanikio niliyopata kwa taifa langu na hakika nitabaki na kumbukumbu nyingi sana kwenye maisha yangu ya soka kwa taifa hili. Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru mashabiki na wafuasi wetu wote. Wao ndio wamefanya haya yote kutokea na ama hakika tumefanikiwa sote."
Bila wao isingekuwa rahisi kutokea haya. Popote nitakapokwenda, nitainadi na kuisimamia bendera ya Sweden."
Kutoka kijana ambaye hapo awali aliishangilia Brazil mpaka kuwa kuwa mshabiki na mnazi namba moja wa Sweden na sasa legend mkubwa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video