Sunday, June 12, 2016

Kikosi cha Yanga kimeondoka kuelekea Uturuki kuweka kambi ya muda mfupi kwa ajili ya kuwavaa Waarabu wa Algeria Mo Bejaia katika mchezo wa kuwania ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika utakaopigwa Algeria June 19.
Yanga imeondoka na kikosi kamili ikiwa ni maandalizi tosha ya kuwavaa waarabu hao kikamilifu.
Katika msafara huo wapo baadhi ya wachezaji muhimu walioachwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo maradhi na kukosa nafasi katika timu.

Kikosi kamili kilichoondoka hiki hapa
▪▪Walinda Mlango.
Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.
▪▪Walinzi.
Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
▪▪Viungo.
Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya.
▪▪Washambuliaji.
Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe.
Msafara umeongozwa na Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh.
- Vicent Bossou ataungana na timu Algeria bado yupo kwao Togo lakini ameomba ruhusa.
-Malimi Busungu majeruhi na Juma Abdul (ni majeruhi aliumia dhidi ya Azam fainali kombe shirikisho)
-Paul Nonga( anaondoka anaweza kusajiliwa Stand United, Benedicto Tinnoco hawapo katika program ya Mwalimu.
-Salum Telela hajaongezewa mkataba (bado mustabali wake haujulikani).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video