Thursday, June 23, 2016

Nawasalimu ndugu zangu wote na kwa wale ndugu, jamaa na marafiki zangu Waislam nawapa hongera kwa kuendelea kutimiza moja ya nguzo zenu muhimu katika Dini hasa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kufunga.

Nimeona niseme yafuatayo kwani natamani sana Timu yangu pendwa Yanga iwe/ipate mtu maalum mwenye weledi wa masuala ya IT na awe na kazi moja tu ya kuendesha Website, Facebook Page, Twitter and Instagram Accounts na hata Play anda Apple Store. 
Mtu huyo awe Idara/Kitengo cha Habari na Mawasiliano chini ya msemaji wake Jerry Muro.

Kwanini nimesema haya sisi bado kwenye mfumo wa kupata habari na matukio kama klabu tuko nyuma sana. 
Tunaendesha mambo yetu kizamani sana na tumerudi hatua 5 nyuma tangu alipoondoka Baraka Kizuguto maana yeye alijitahidi kwa sehemu fulani. 
Msemaji wetu Jerry Muro ni hodari sana kwenye media hasa TV na Radio ila kwenye masuala ya Kimtandao, niseme wazi bado hajawa sawia kabisa licha ya uzoefu na taaluma yake kwenye tasnia hiyo. 
Mfano kule fb anatumia Account ambayo sio PAGE na hii aliianzisha yeye na sio mali ya klabu, lakini bado Account hiyo haijawa makini na kuangalia nini cha kupost hasa chenye tija na manufaa kwa klabu na kumekuwa na mkanganyiko wa taarifa zihusuzo klabu yetu ,tukumbuke account binafsi mwisho ni watu 5000 na zaidi utapata followers ambao hawatakuwa na fursa ya kuchangia comments zao. 
Mfano huo pia ni sawa na Account ya Instagram ambayo imekaa kibinafsi sana na haiko updated. 
Ukienda kwenye suala la website ya klabu ndio hakuna jipya alafu tunajiita wa Kimataifa kisa tunashiriki International Tournament  lakini kwenye masuala ya Teknolojia ya Habari tupo kule kule kwa miaka ya mwanzoni mwa 2000.
Hapa ni kusema website ya Yanga haiko hai wala kibosho ni imekufa.

Jiulize tu leo timu ilikuwa Kambini Uturuki kisha ikaenda Algeria na imerudi Uturuki tunapata wapi baadhi ya matukio kutoka kwa wachezaji na baadhi ya viongozi walioko kule? Kama sio kupitia Accounts zao binafsi za mitandao ya kijamii.... HII NI AIBU KUBWA SANA. 
Je matukio mbalimbali za mechi kama ile timu ya Mauritius, APR, AL AHLY na hivi karibuni mechi za Sagrada na hii ya juzi ya MO Bejaia tunayapata wapi sisi kama wanachama na mashabiki na wapenda soka ulimwenguni kote ambao ni wadau wa Yanga ? 
Nendeni kwenye Website au Facebook Pages ya MO Bejaia mkaone walivyoripoti na kuweka matukio ya mchezo huo ndivyo walivyofanya Al Ahly na timu nyingi za Barani Afrika kama TP Mazembe, Zamalek, Mamelodi Sundowns n.k
Hivi tunaweza kujitangaza na kupata wadhamini mbalimbali kama tumejifungia ndani?......LAZIMA TUTOKE NJE NA KUJITANGAZA. 
Hata kupitia hiyo website au blog tunaweza kupata wadhamini  wa kuziendesha hizo Accounts.

Tusikatae kujifunza na kama mtu ninayependa kuwa kwenye mitandao ya Kijamii basi AZAM FC ni darasa tosha sana hasa namna mfumo wao wa kupata taarifa huku kwenye Social Media. 
AZAM FC utawapenda kuanzia Website yao, Facebook Page na Instagram wao wanaripoti masuala ya timu yao na zile za vijana kuanzia usajili, mazoezi, mechi, safari  na programmes nyingine nyingi.
Hata klabu ndogo kama Mbeya City wametuacha sana kwenye hatua hii sembuse mtani wetu wa jadi Simba ambao nao wanajitahidi licha ya kujikongoja kama mzee mwenzake.

Naomba niseme sasa kuwa Yanga ni Klabu kubwa ambayo pia ni Taasisi hivyo haiwezekani alipokuwa Sendeu kama msemaji basi nae alkuwa na Accounts zake za kucontrol huku kwenye mitandao ya kijamii, Pia alipokuja Kizuguto ikawa hivyo hivyo na sasa yupo Jerry Muro nae anaendesha kwa utaratibu wake. 
Ifikie hatua tujipambanue sasa kama klabu kongwe na yenye kuliteka soka la Afrika kwa kuwa na mpango maalumu kwenye Idara hiyo wa kutoa habari kwa njia ya mtandao ili watu wote ulimwenguni wapate na kuzisoma kwa wakati. 
Pia tutumie Accounts hizo kwa mambo ya klabu pekee na yahusuyo timu yetu na sio vinginevyo au binafsi.
Tuweke utamaduni wa kuziendesha accounts za klabu kwa muendelezo kama leo yupo X basi akija Y yeye apate jukumu la kubadilisha Password tu.

Narudia tena ni aibu kuzipata habari za Yanga kwenye blogs za SALEH JEMBE, BOIPLUS, BIN ZUBEIRY, KANDANDA TZ, SOKA 360, SHAFFIH DAUDA n.k....  na kupitia Accounts binafsi za Wachezaji na Viongozi wanapokuwa sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Rai yangu kwa viongozi waliochaguliwa na hasa wajumbe wa Kamati ya Utendaji kaeni na Sekretarieti mkiwa na viongozi wa juu kuangalia namna ya kuwa na Strong network katika Social Media..... WEBSITE, FACEBOOK PAGE, INSTAGRAM na TWITTER. 
Shirikianeni na Msemaji wetu Jerry Muro kuona namna gani tunaondokana na uzamani huu katika maisha ya kisasa. 
Ndugu zangu wajumbe wa Kamati ya Utendaji wakina Samwel LUKUMAY, Salum MKEMI, Thobias LINGALANGALA, Siza LYIMO, Hashim ABDALLAH, Hussein NYIKA, Ayoub NYENZI na AMEIR nyie hamshindwi kwa umoja wenu kumtafuta kijana mmoja ambaye ni mwana YANGA  na kumpa ajira ya kuziendesha hizo Accounts chini ya uangalizi na uratibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya Klabu. 
Pia kuhakikisha kijana huyo anaenda kokote kule ambako Timu ipo pia anakuwa na vifaa vya kisasa vya kufanyia shughuli hiyo kama Camera, Laptop, Modem, Ipad n.k
Na awe mahiri kwenye lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa kupeleka taarifa za klabu kwenye Google(Wikipedia, the free encyclopedia) zinazohusu Klabu nzima kuanzia Uongozi, Wachezaji na Benchi la Ufundi.

Leo nimeona niyaandike hayo kama sehemu ya kuuweka Moyo wangu huru juu ya kadhia hii ambayo haipaswi na haitakiwi kuwepo kwa Timu inayojiita ya KIMATAIFA maana nilikuwa najiona mzito nisiposema ukweli wa jambo hili.

ANGALIZO: Nimepata taarifa kuwa tunahitaji kuingia mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya MACRON au kama wengine wanavyosema kuwa kampuni hiyo ndio wadhamini wakuu kwa upande wa vifaa vya michezo kwenye hatua hii ya 8 Bora katika Makundi ya Kombe la CAF CONFEDERATION CUP. 
Angalizo langu ni kwa viongozi, wachezaji na benchi la ufundi tuwe makini sasa hasa kwa kuchanganya baadhi ya bidhaa/nembo za makampuni mengine ya vifaa vya michezo. 
Huwezi ukavaa Fulana au Suti ya Michezo yenye nembo ya MACRON kisha ukabeba begi la Umbro, Nike au Puma kisha chini ukavaa raba au sendozi za kampuni ya Kappa au Addidas. 
Maana kama MACRON wana haki hiyo tuwape haki yao kwenye vifaa vya michezo nje ya udhamini wetu mwingine ambao Klabu itaingia na makampuni mengine kwa ajili ya kutangaza biashara zao kama ilivyo sasa kwa kampuni ya Bia ya TBL kupitia Kilimanjaro Lager.

Mwisho najua kwa namna moja au nyingine nitakuwa nimewakwaza baadhi ya watu, kuandika majina ya watu, blogs nilizozitaja bila lidhaa yao basi naomba mkanisamehe tena bure kwani hii yote ni kutaka kuona YANGA tunajipambanua kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO.
Wasalaam,
Junior Matukuta
Mbeya.
+255 762 047686 

Facebook: Junior Matukuta 
Twitter: @Malanyingi 
Instagram: @Matukutajr

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video