Wales wameanza kwa kicheko michunao ya Euro 2016 inayofanyika nchini Ufaransa baada ya kuwanyuka Slovakia kwa mabao 2-1, mchezo wa kundi B uliofanyika kunako dimba la Matmut Atlantique huko jijini Bordeaux.
Wales ambao wamekosekana katika michuano mikubwa duniani kwa miaka 58, walianza kupata bao lao kupitia kwa nyota wao anayekipiga Real Madrid Gareth Bale kwa faulo nzuri na kutinga wavuni na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli moja.
Slovakia walisawazisha bao kupitia kwa nyota wao Ondrej Duda dakika ya 61, kutokana na pasi nzuri ya Robert Mak baada ya kutumia vizuri makosa ya walinzi wa Wales.
Lakini alikuwa ni Hal Robson-Kanu, ambaye aliingia kutokea benchi na kuifungia Wales goli la ushindi mnamo dakika ya 81, baada ya kupokea pasi mujarab kutoka kwa Aaron Ramsey.
Matokeo haya yanawafanya Wales kukaa kileleni mwa kundi B na kuwaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya mtoano. England nao wapo dimbani wakichuana na Urusi.
Vijana hao wa Chris Coleman watakutana na England Jumanne ijayo kwnye mchezo wa pili wa kundi B.
Dondoo muhimu za kufahamu
- Mpira wa adhabu wa Bale uliozaa goli ni shuti lake kwanza kulenga lango akiwa na Wales katika michuano hii ya Euro.
- Bale alifunga goli lake la kwanza akiwa na Wales pia katika mchezo dhidi ya Slovakia Oktoba mwaka 2006. Goli hilo pia lilitokana na mpira wa adhabu.
- Ondrej Duda alifunga goli katika sekunde ya 52 baada ya kutokea benchi, goli la haraka zaidi kufungwa na mchezaji aliyetokea benchi katika michuano hii, lilifungwa na Juan Carlos Valeron wa Uhispania kwenye mchezo ya dhidi ya Russia mwaka 2004 (lilifungwa katika sekunde ya 39).
- Wales wameruhusu goli katika kila mchezo kwenye michezo yao yote mitano ya mwisho (ukijumlisha na ya kirafiki), ukiwa ni mwenendo mbaya tangu walipofanya hivyo March 2013 (mara 11).
- Wales imekuwa ni sehemu ya kwanza Uingereza kushinda katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Euro mwaka huu
- Ramsey amehusika katika magoli matatu ya Wales kwenye michezo mitatu iliyopita (magoli mawili na pasi ya goli moja).
0 comments:
Post a Comment