Friday, June 17, 2016

Wakati Dunia ikienda mwendokasi,maisha nayo yakienda mwendokasi ,vijana wakiwa wa mwendokasi  na vyakula ni vya mwendokasi vilevile.
Hii ni baada ya Tanzania  kuleta usafiri wa mwendokasi  kwa maana ya usafiri wa haraka ili kurahisisha safari za ndani ya jiji la Dar-es-salaam  kwa maana ya kuondoa kadhia ya foleni katika jiji hili.
Haimaanishi kwamba mwendokasi upo katika usafiri tu ,la hasha bali upo hata katika  soka kutokana na ushindani wa wachezaji katika kuchukua makombe katika timu zao Taifa hadi katika vilabu vyao wanavyovichezea ili kujirahisishia njia ya kushinda tuzo mbalimbali kama ;kiatu cha mfungaji bora wa ligi husika na mchezaji bora wa Dunia.
Leo katika makala yetu tutazungumzia namna ambavyo  wachezaji wakisinzia tu tuzo  inapanda mwendokasi.

1.CRISTIANO RONALDO [CR 7.]
Huwezi kuamini kama ni kweli kwamba naye akisinzia tu tuzo inapanda mwendokasi kutokana na kushinda kombe la Klabu Bingwa Ulaya na vilevile kutwaa tuzo ya mfungaji bora katika michuano.
Lakini ni tofauti kidogo na fikra za wengi kutokana na kwamba,  kombe na tuzo alizotwaa zimemfungulia njia nzuri ya kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Dunia lakini si kwa asilimia nyingi kwasababu  kuna michuano ya Euro,  ambayo timu yake ya Ureno inashiriki kwahiyo inaweza kumuongezea asilimia kama akitwaa kombe hilo au kuifikisha katika nafasi nzuri katika michuano hiyo ama kumpunguzia asilimia za kutwaa tuzo hiyo.
Mchezaji huyo bora wa Dunia mara tatu kama akibahatika kutwaa tuzo hiyo atakuwa amewapita wachezaji wa zamani kama ; Zinedine Zidane, Ronaldo De Lima, Michel Platin, Marco Van Basten na marehemu Johan Cruyff ambao nao wametwaa mara tatu .
Kama akitwaa tuzo  hiyo inamaanisha kwamba atakuwa na tuzo nne na hivyo kupunguza umbali baina yake na hasimu wake Lionel Messi aliyetwaa mara tano.

2. LIONEL MESSI [LA PULGA.]
Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kwamba naye akisinzia tu tuzo inapanda mwendokasi kwa upande wake ijapokuwa ametwaa makombe mawili ambayo ni La Liga  na Kombe la Mfalme (Copa de Rey).
Vivyo hivyo, kwa upande wake inamuwia ugumu kutokana na kwamba si kazi rahisi kutwaa ilhali kuna wapinzani ambao wameshajiwekea mazingira mazuri  katika kutwaa tuzo hiyo , na vilevile kama akibahatika kutwaa kombe la Copa America linaloendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali nchini Marekani litamuongezea asilimia za kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo na kama akishindwa itampunguzia asilimia za kutwaa tuzo hiyo kwa mara nyingine .
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona ya Hispania kama akitwaa tuzo hiyo atakuwa yuko mbele zaidi ya wachezaji wote Duniani kama  Cristiano  Ronaldo na wengine wengi ambao wamewahi kutwaa tuzo  hiyo.

3. LUIS SUAREZ.
Kwa huyu naye ni vivyo hivyo kwasababu ana wakati mgumu kutoka kwa washindani  wake ijapokuwa ametwaa tuzo ya mfungaji bora wa La Liga na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri  ya kushindania tuzo hiyo.
Lakini kwa upande mwingine ana wakati  mgumu mno  kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika mashindano ya Copa America  kutokana na kutolewa nje ya michuano hiyo.
Mchezaji  huyo wa Uruguay na klabu ya Barcelona kama akitwaa tuzo hiyo atakuwa ni mchezaji  wa kwanza tofauti ya Messi na Ronaldo  ndani ya miaka nane kutwaa tuzo hiyo .  

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video